
Vidole vya binadamu vikiwa vimeshikilia ganda la risasi baada ya kutumika.
Watu wawili wanadaiwa kupigwa risasi na mmoja kujeruhiwa vibaya huko Makunduchi kwenye uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Waliojeruhiwa ni pamoja na Kheri Makame Hassan (42), Ramadhan Hijja Hassan (29) na Ali Seif Issa (38) huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Unguja, Juma Saadi akieleza kutokuwa na taarifa za watu kupigwa risasi.
Kamanda huyo alieleza kuwa taarifa zilizomfiki mezani kwake kuwa risasi ilipigwa juu kwa bahati mbaya.
Dk Seif Suleiman wa Hospitali ya Al Rahma amethibitisha kupokea majeruhi na kusema kuwa anasubiri picha za X Ray ili kujua majeraha hayo yametokana na nini.
Katika uchunguzi wa awali umeonesha kuwa majeraha hayo huenda ikawa ni risasi kutokana na kuwacha uwazi katika miili yao.

Hadi sasa majeruhi hao wamelazwa katika hospitali ya Al Rahma wakipatiwa matibabu ambapo mmoja ikidaiwa kuwa hali yake ni mbaya.Chanzo kutoka kwa Mwandishi Mkongwe Visiwani Zanzibar, Salma Said

0 comments:
Post a Comment