BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SHERIA MPYA YA KUSHIKA MIMBA KWA KUPATA RUHUSA YAPITISHWA, MWANAMKE AKISHIKA MIMBA BILA RUHUSA KUTOZWA FAINI NCHINI CHINA.

Mwakamke mja mzito China 
Kampuni moja ya Uchina inapanga kutoa masharti ambapo wafanyikazi wake watatakiwa kupata ruhusa kabla ya kuanza familia.

Sheria hizo zimechapishwa na kuzua malalamiko mengi katika mitandao.


Sheria kuu inaelezea kwamba wanawake wote walio kwenye ndoa lazima wawe wamehudumu kwa mwaka mmoja kwenye kampuni hiyo kabla ya kutuma kibali cha kukubaliwa kushika mimba yeyote na atakayeshika mimba kinyume cha sheria hiyo atatozwa faini na kunyimwa madaraka yoyote, hata kama amefuzu.

Shirika la utangazaji nchini China limekosoa vikali kampuni hiyo iliyoko mkoa wa Henan na kusema haina ubinadamu kwa wafanyikazi wake.

Muingilio wa masuala binafsi China ni jambo rasmi, hasa sheria ya mtoto mmoja iliyowekwa na serikali miaka ya sabini. Hii iliwalazimisha wazazi kupata mtoto mmoja pakee.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: