Waumini wa dini ya kiislamu wakisikiliza hutuba ya swala ya Edd El Fitr iliyokuwa ikisimwa na Shekhe Abdallah Mkangambe (hayupo pichani) katika mskiti mkuu wa mkoa, baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mkutufu wa ramadhani, mtaa wa Boma Road Manispaa ya Morogoro.PICHA ZOTE NA MTANDA BLOG
Shekhe Abdallah Mkangambe akisoma hutuba ya swala ya Edd El Fitr katika msikiti kuu wa mkoa wa Morogoro kwa waumini wa dini ya kiislamu (hawapo pichani)
Omari Hussein Mkwizu na Juma Mtanda wakiwa katika sehemu nyingine ya waumini wa dini hiyo wakisikiliza mawaidha muda mfupi kabla ya swala ya Edd El Fitr kuswaliwa katika msikiti mkuu wa mkoa wa Morogoro Boma Road.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Rajabu Rutengwe akizungumza jambo na waumini wa dini ya kiislam wakati wa swala ya Edd El Fitr katika ibada iliyofanyika kwenye msikiti mkuu wa mkoa, baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mkutufu wa ramadhani, mtaa wa Boma Road Manispaa ya Morogoro.
Hapa Mkuu huyo wa mkoa wa Morogoro Dkt Rajabu Rutengwe akijumuika na waumini hao kuomba dua.
Safi ya mashekhe kushoto wakitakiana heri ya sikukuu ya Edd El Fitr baada ya kumalizika kwa swala hiyo iliyofanyika kimkoa katika msikiti mkuu wa mkoa wa Morogoro.

0 comments:
Post a Comment