BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MASHINDANO YA LIGI YA ULINZI SHIRIKISHI CUP 2015 YAANZA KUVURUGA NYASI UWANJA WA JAMHURI MOROGORO.

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Sabasa City, Victor Mswaki akimtoka mlinzi wa Moro Kids Nickson Sudan wakati wa ligi ya mashindano ya Ulinzi Shirikishi Cup 2015 katika michezo inayoendelea kufanyika uwanja wa Shujaa mkoani Morogoro. katika mchezo huo Moro Kids ilifungwa bao 3-1.
Juma Mtanda.


Na Juma Mtanda, Morogoro.

Timu tano zinazoshiriki mashindano ya ligi ya Ulinzi Shirikishi Cup 2015 ya mtoano zimefuzu hatua ya 16 bora baada ya kushinda michezo yao inayoendelea kufanyika katika uwanja wa Shujaa Manispaa ya Morogoro.


Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Msimamizi wa mashindano hayo ambaye ni Katibu Mkuu Mtendaji wa chama cha soka Manispaa ya Morogoro, (MMFA) Kafale Maharagande alisema michezo ya mashindano hayo yalianza kutimua vumbi Agosti 18 huku timu tano zikifanikiwa kufuzu kucheza hatua ya 16 bora baada ya kufanya vizuri katika ligi hiyo inayoendeshwa kwa mtoano.


Maharagande alisema kuwa katika mchezo wa ufunguzi timu mwenyeji wa mashindano hayo, Polisi Veteran FC walipata ushindi ikihusisha changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya kuiondoa Chamwino Rangers kwa kupata bao 4-2 kufuatia kumalizika kwa dakika 90 kutoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1.


Mshambuliaji Fikiri Hussein (Mmachinga) wa Polisi Veteran ndiye aliyeokoa jahazi la timu yake lisizame na kufufua matumaini mapya kwa kufunga bao la kusawazisha dakika ya 54 huku golikipa Emmanuel Mwasika akiokoa mikwaju miwili ya penalti mbili.


Msimamizi huyo alitaja michezo mingine kuwa timu ya Uhuru Rangers iliyofanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuicharaza Sultan Rangers kwa kuifumua bao 2-1 huku mabao ya washindi yakididimizwa wavuni na Ally Koyi aliyefunga yote mawili wakati la Sultan lilifungwa na Funga Salehe.


Timu ya Vijana wa Moro Kids chini ya umri wa miaka 20 walikiona cha mtema kuni kilichomfanya kanga kuota na madoa kufuatia kutandikwa bao 3-1 na timu ya Sabasaba City katika mchezo mkali wa michezo hiyo.


Sabasaba City ilianza kuhesabu kalamu ya mabao dakika ya tatu na 17 kupitia kwa Donald Ngosha aliyefungwa mabao yote kwa mikwaju ya penalti iliyotolewa na mwamuzi chipukizi Erick Daud baada ya wachezaji wa Moro Kids kufanya madhambi katika eneo la hatari katika huku Baraka Thoufil alihitimisha kalamu ya ushindi huo kwa kufunga bao la tatu katika dakika ya 59 wakati lile la kufutia machozi la Moro Kids likifungwa na Boniface Joseph dakika 63.


Black People iliisambaratisha timu ya kanisa la Anglikana FC kwa kuifunga bao 3-0, mabao yaliyofungwa na washambuliaji, Muhamad Rajab, Salehe Jirani na Gerad Mdawi.


Wakati Black People ikipata ushindi huo timu ya Sansiro yenyewe ilitolewa nishai na Chipolopolo kwa kufungwa bao 5-4 kwa njia ya penalti baada ya kumalizika kwa dakika 90 bila kufungana.


Maharagande alisema kuwa mashindano hayo yanashirikisha jumla ya timu 32 na yatapitia katika hatua sita ikiwemo ya makundi, 18 bora, 10 bora, robo fainali, nusu fainali, mshindi wa tatu na fainali yenyewe itayochezwa Septemba 21.


"Mashindano haya yatasaidia kuimarisha viwango vya wachezaji wanaoshiriki ligi mbalimbali zinazoandaliwa na wilaya na mkoa lakini wakati huo huo wapenda soka watapata fursa ya kushughudia burudani kutoka katika mashindano haya."alisema Maharagande.


Maharagande alisema kuwa michezo hiyo imezinduliwa rasmi Agosti 18 ambapo hatua ya makundi inatarajia kumalizika Septemba 03 wakati timu zitakazoingia 18 bora zitachuano hadi kuanzia Septemba 06 hadi 14 huku Septemba 17 hadi 21 zitakutana timu zilizofuzu kuingia hatua ya 10 bora.


Alieleza kuwa ratiba hiyo inaonyesha kuwa robo fainali itafanyika Septemba 24 hadi Septemba 26 wakati nusu fainali itakuwa kati ya Septemba 29 hadi 30 huku mshindi wa tatu akisakwa Oktoba 02 na fainali ikipigwa Oktoba mwaka huu.


Timu zinazoshiriki katika michezo hiyo ni pamoja na Uhuru Rangers,Sultan Rangers, Chamwino Rangers, Polisi Veteran FC, Moro Kids, Sabasaba City, Black People FC, Anglikana Compossion, Jamaica FC, Mwere Kids na Kingaru United.


Nyingine ni pamoja na Mlunda FC, Uluguay FC, Maskani FC, Cida Estate FC, Mkundi United, Moro Veteran, Madagu FC, Hot Stars, Kaizer Chief FC, Santos FC, Msamvu Terminal FC, Tubuyu FC, Liti FC, Black Viba, G. Seven FC, Kihonda Magolofani FC, Dundee FC. Na Moro City FC.


Maharagande alisema kuwa zawadi ya mshindi wa kwanza atakabidhiwa seti ya jezi na mpira mmoja huku mshindi wa pili akipata mipira mitatu, watatu ataambulia zawadi ya mpira miwili.


Kwa upande wa wachezaji bora mchezaji bora na golikipa bora wenyewe kila mmoja wataondoka na zawadi ya fedha taslimu kiasi cha sh50,000.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: