BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MZIMU WA KUTWANGANA MAKONDE SASA WAHAMIA CHADEMA KATIKA MKOA WA SONGEA.

WAFUASI wa CHADEMA, waligeuza eneo la Mahakama Kuu ni la kuoneshana ubabe baada ya kukunjana na kupigana kabla ya kesi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe jijini Dar es Salaam katika picha ya maktaba.

 Wakati mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge katika vyama mbalimbali vya siasa ukielekea ukingoni, wananchama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jimbo la Songea Mjini, wamerushiana makonde na kusababisha mtafuruku.

Hatua hiyo imesababisha Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Songea, John Mwankina na mgombea udiwani kata ya Tanga, Musa Ndomba, kupigwa na baadhi ya wafuasi.

Habari zilizothibitishwa na Mwankina zimeeleza kuwa vurugu hizo zilianza Agosti 21, saa 2:30 na kudumu hadi saa 4 usiku kwenye ofisi ya chama hicho baada Ndomba kudai kuwepo makundi ndani ya chama na kusababisha kushindwa kwenye uchaguzi mkuu.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.

Taarifa zaidi za tukio hilo zimeeleza kuwa muda mfupi baada ya kumaliza mchakato wa kura za maoni ya udiwani na ubunge kwa baadhi ya wagombea ambao walishindwa, waliamua kukata rufaa kupinga matokeo hayo kwenye kata za Majengo, Tanga, Msamala na Matarawe na kuwa rufaa hizo zilipelekwa moja kwenye ngazi ya mkoa ambako baraza la wazee wa chama hicho lilipokea na kuzifanyia kazi.

Taarifa zilidai kuwa baadae baraza la wazee lilitoa mapendekezo kwa kamati ya utendaji ya chama ya wilaya ya Songea kuwa maamuzi yatakayotolewa na kamati ya utendaji yafuatwe na kuzingatia ushauri uliotolewa na baraza hilo.

Mgogoro huo ulifikia hatua ya kuanza kupigana na kumfungia ndani ya ofisi katibu wa chama wa wilaya hiyo, Olais Cheenga, ambaye baadae alilazimika kumpigia simu Mwenyekiti wa Chadema wa wilaya, aliyekuwa mbali na eneo hilo ambaye alifika na kukuta kikundi cha ulinzi cha chama hicho cha Red brigade kikiwa kimezingira eneo hilo.

Taarifa zinaeleza kuwa mwenyekiti huyo alijikuta akipigwa na kikundi hicho cha ulinzi kisha kumfuata Ndomba aliyekuwa amesimamisha gari karibu na eneo hilo na kumpiga yeye na dereva wake.

Ndomba aliwaambia waandishi wa habari aliamua kuandika barua kujiengua kugombea udiwani baada ya kuona kundi la mgombea ubunge linakikuka kanuni na taratibu za ndani ya chama.

Naye mgombea ubunge Jimbo la Songea mjini kupitia chama hicho, Joseph Fuime, alipoulizwa kuhusiana sintofahamu hiyo ndani ya chama alikanusha kuhusika na mgogoro huo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela, amesema polisi halijapokea taarifa za tukio hilo licha ya kupata kupitia vyombo vingine.CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: