BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAHAKAMA KUU KANDA YA MOROGORO YAWAHUKUMU KIFUNGO CHA MIAKA 15 JELA MARIAMU NA MTONGA KWA KUMUUA MTOTO NASRA MVUNGI (4) (MTOTO WA BOKSI) .


Nasra Mvungi enzi za uhai wake.

By Hamida Shariff, Mwananchi
Morogoro. Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro, imewahukumu watu wawili kutumikia kifungo cha miaka 15 jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila ya kukusudia Nasrah Mvungi maarufu kama ‘mtoto wa boksi’ wakati akiwa na umri wa miaka minne.

Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mtoto Nasra Mvungi, Omar Mtonga akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi wakati wa kesi yake mahakama ya hakimu mkazi Morogoro.

Jaji Elieza Mbuki alitoa hukumu hiyo jana baada ya kuwatia hatiani washtakiwa hao Mariamu Said (39) na mumewe Omar Mtonga kutokana na ushahidi ulitolewa mahakamani hapo kuthibitisha bila kuacha shaka kuwa walitenda kosa hilo.

Jaji Mbuki alisema mahakama hiyo imeridhishwa na ushahidi huo uliotolewa na upande wa mashtaka na kuwatia hatiani washtakiwa hao kisha kuwahukumu kifungo hicho jela ili iwe fundisho kwao na kwa watu wengine wenye tabia kama zao.

 
Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mtoto Nasra Mvungi, Mariam Saidi akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi wakati wa kesi yake mahakama ya hakimu mkazi Morogoro.
 Washtakiwa hao na baba wa mtoto huyo, Rashid Mvungi walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza na kusomewa mashtaka ya kula njama na kufanya vitendo vya kikatili dhidi ya Nasrah.
Baba Mzazi wa Nasra, Rashidi Mvungi (kushoto) akiwa mahakamani na watuhumiwa Mariam Said na mumewe Omary Mtonga katika moja ya usikilizaji wa kesi yao.

Mwanasheria wa Serikali, Janeth Kisibo alidai washtakiwa hao, walitenda makosa hayo Desemba 2010 na Mei 2014 na kuathiri afya ya mtoto huyo.

Alidai shitaka hilo lilibadilika kuwa la mauaji baada ya Nasrah kufariki Juni Mosi, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikolazwa kwa matibabu. Wakati kesi hiyo ikiendelea, mshtakiwa wa tatu aliachiwa huru.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: