BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BREAKING NEWS: CCM YASHINDA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 KWA DK JOHN MAGUFULI KUWA RAIS WA TANO WA TANZANIA.



Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha CCM John Pombe Magufuli ndiye rais mteule wa taifa la Tanzania baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliokamilika.

Akitoa matokeo hayo Mwenyekiti wa tume hiyo jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Magufuli alijipatia kura milioni 8,802,935 ikiwa ni aslimia 58.46 huku mpinzani wake wa karibu Edward Lowassa wa chama cha Chadema

akijipatia kura milioni 6,072,848 ikiwa ni aslimia 39.97.

Haya ndiyo matokeo kamili kama yalivyotangazwa na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva:
 
Matokeo ya uchaguzi wa urais Tanzania
Jina Chama Kura Asilimia
Anna Mghwira ACT 98,763 0.65
Chifu Yemba ADC 66,049 0.43
John Magufuli CCM 8,802,935 58.46
Edward Lowassa CHADEMA 6,072,848 39.97
Hashim Spunda CHAUMA 49,256 0.32
Janken Kasambala NRA 8,028 0.05
Macmillan Lyimo TLP 8,198 0.05
Fahmi Dovutwa UPDP 7,785 0.05  


Awali kabla ya kutolewa kwa matokeo hayo Takriban vyama vitano kati ya vinane viliridhia kutia sahihi matokeo hayo ambayo tayari yamepingwa na chama rasmi cha upinzani CHADEMA.

Akivihutubia vyombo vya habari mgombea wa urais kupitia chama hicho Edward Lowassa amepinga matokeo yoyote ya uchaguzi huo na kujitangaza mshindi wa uchaguzi kwa kupata asilimia 62 ya kura zilizopigwa.

Lowassa amedai kwamba tume ya uchaguzi nchini humo imeshirikiana na chama tawala CCM kufanya udanganyifi katika shughuli hiyo.

Lakini akitoa matokeo hayo Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa baada ya kujumlisha matokeo yote ya urais katika uchaguzi huo,John Pombe Magufuli ndiye aliyeibuka mshindi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: