
Na Marthia Canal Wa Iramba.
MATOKEO YA MKOA WA DSM YANATOSHA KUMTANGAZA MAGUFULI MSHINDI.
Matokeo ya mkoa wa Daresalam yananifurahisha kuliko yanavyowafurahisha UKAWA. Wamekuwa wakiyashangilia ila wanashindwa kuyaangalia kwa jicho la kitafiti. Ngoja niwaonyeshe kitu hapa.
MATOKEO YA MKOA WA DSM YANATOSHA KUMTANGAZA MAGUFULI MSHINDI.
Matokeo ya mkoa wa Daresalam yananifurahisha kuliko yanavyowafurahisha UKAWA. Wamekuwa wakiyashangilia ila wanashindwa kuyaangalia kwa jicho la kitafiti. Ngoja niwaonyeshe kitu hapa.
Ipo
hivi Mkoa wa Daresalam ndio mkoa uliokuwa na wapiga kura wengi kuliko
mikoa yote tanzania walikuwa wamejiandikisha watu 2,000,000+ hakuna mkoa
uliokuwa na idadi kubwa ya wapiga kura namna hii hapa nchini hilo lipo
wazi.
Wagombea wote walikuwa wanaujua
mtaji huu hivyo waliwekeza zaidi kwenye mkoa huu. Ukawa ndio waliokuwa
wamewekeza zaidi kwenye mkoa huu ila matokeo ya uchaguzi huu hauendani
na uwekezaji waliouwekeza. Kwa maana hiyo Daresalam ni mkoa ambao
ulikuwa unategemewa sana na ukawa na Lowassa kila weekend alikuwa
anarudi Dar kufanya Kampeni.
Ikumbukwe
kwamba mpaka matokeo ya mchana wa leo kutoka tume Magufuli alikuwa na
kura 1,687, 752 huku Lowassa akiwa na kura 1,215,555 hapa Magufuli
amemzidi Lowassa kwa kura 472,198. Nilikuwa nasubiri mkoa wa Daresalam
kama wanaweza kulipunguza hili gape wafuasi wamebaki kushangilia kina
Kubenea bila kujua matokeo yale yamebeba nini.
Ngome pekee waliyobaki nayo Chadema ni Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha tu hii ni hatari kwao.
Sassa
tuyachambue matokeo ya mkoa wa Daresalam ili uelewe naongea nini. Mkoa
wa DSM ulikuwa na majimbo 10 hapa nitatoa mchanganua ambao Ukawa
wamenyakua majimbo na jimbo moja tu la CCM, Yale mengine ya ambako CCM
imeshinda sitayazungumzia kwa kuwapendelea kabisa wana Ukawa hayo
sitayaweka hapa , kama wapiga kura zaa wabunge walimchagua pia raisi
mambo yangekuwa hivi:-
1.TEMEKE:- UKAWA Kura 103,231 CCM kura 97,555
2. KAWE: - UKAWA Kura 96,432 CCM Kura 83,061
3. UBUNGO:- UKAWA Kura 87,606 CCM Kura 59,514
4. ILALA:- UKAWA Kura 32,533 CCM Kura 35,818
5. KIBAMBA:- UKAWA Kura 79,274 CCM Kura 55,410
Ukichukua
jumla ya Kura za UKAWA hapo unapata jumla ya kura 399,076 na za CCM
kura 367,830 ukitafuta tofauti ya kura kwa majimbo haya utaona UKAWA
wanazidio la kura 31,346 tu kwa majimbo yote matano hapo juu yamebaki
majimbo mengine 5 ambayo 3 CCM wameyashikilia nayo ni Kigamboni,
segerea, na Kinondoni.
Ukichkua 31,346
ya zidio la kura hizi za ukawa ukajumlisha na zile za Lowassa hadi
mchana wa leo utapata kura 1,246,801 Magufuli muachie zile zile za
mchana 1,687, 752 ukitoa hapo Magufuli anakuwa na zidio la kura 440,951.
Narudia hapa sijaweka majimbo 3 mengine waliyoshinda ccm nimeweka moja
tu la Ilala.
Kama Ukawa wameshindwa
kutumia fursa ya mkoa huo wa Daresalam wanasubiri ushindi wapi? Arusha
na Kilimanjaro inaweza kushindana na Kanda ya ziwa?
Kuna
uwezakano mkubwa sana kuwa mtu alimchagua Kubenea ila uraisi akampa
Magufuli hilo linawezekana hivyo tarajia makubwa hapa inawezekana
Magufuli akawa na kura nyingi kuliko Lowassa kwenye Mkoa huu.
Ukawa hapa mmepigwa jipangeni kwa 2020 kwani hata huko Arusha na Kilimanjaro mmekabana sana.
Hiki
ni kichapo kwa wale wazee wa statistics watanielewa hapa nikipata
matokeo ya Arusha tu nitakuwa nimeshajua Magufuli atashinda kwa Asilimia
ngapi.
KUTOKA MITANDAO YA KIJAMII OKTOBA 29, 2015
KUTOKA MITANDAO YA KIJAMII OKTOBA 29, 2015

0 comments:
Post a Comment