BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MGOMBEA URAIS WA UKAWA EDWARD LOWASSA AWAOMBEA KURA YA NDIYO WAGOMBEA WA UBUNGE NA UDIWANI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) IFAKARA MKOANI MOROGORO.

Mgombea Urais Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anaeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa akihutubia mkutano wa hadhara katika jimbo la Mikumi mkoani Morogoro jana. 

MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeungwa mkono na mwavuli wa Ukawa, Edward Lowassa, amejikuta akiombea kura wabunge na madiwani waliosimamishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza katika kampeni zake Ifakara mkoani Morogoro jana, zinazotarajiwa kuhitimishwa leo jijini Dar es Salaam, Lowassa aliomba wananchi wampigie kura ya urais yeye, lakini madiwani na wabunge wapewe wa CCM.

Kutokana na kauli hiyo iliyotolewa mbele ya umati wa watu, huku mkutano huo ukirushwa moja kwa moja na moja ya televisheni kubwa hapa nchini, baadhi ya viongozi wa Ukawa walichukua kipaza sauti na kumpa muda wa kutafakari, kabla ya kuendelea kuomba kura.

Hali hiyo ambayo haikutarajiwa na wengi ambayo pia haikutolewa ufafanuzi, ni sehemu ya baadhi ya matukio yasiyotarajiwa ambayo yamekuwa yakimtokea mgombea huyo.

Mwishoni mwa wiki hii, alipokuwa katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Lowassa alipotakiwa kueleza namna atakavyopambana na ufisadi katika ngazi ya juu, kwa maana ya rushwa kubwa, alijikuta akisema ufisadi ni swali gumu.

Akifafanua zaidi Lowassa alisema swali hilo mbali na ugumu, lakini pia ni refu na lingetaka kuwa na mjadala wake peke yake, huku akisema katika rushwa ndogo, baada ya kutafakari ameona kwa kuanzia ni kuwa na kituo kimoja cha kutoa huduma zote za Serikali, ili kupunguza urasimu.CHANZO:HABARILEO.
Lowassa akiteta jambo na Mgombea Ubunge wa Chadema, Jimbo la Mikumi, Joseph Haule 'Prof J'.Picha/mrokim.blogspot.com



Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: