BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAMANDA WA POLISI AAGIZWA KUKOMESHA TABIA YA ASKARI POLISI KUSHIRIKIANA NA MAJAMBAZI KUFANYA UHALIFU, NI AIBU TUPU.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ludovick Mwananzila

Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ludovick Mwananzila amemuagiza kamanda wa polisi mkoani hapa, Hamis Issa kuhakikisha hakuna askari anayejihusisha au kushirikiana na wahalifu.

Hatua hiyo inatokana na baadhi ya askari kutuhumiwa kushirikiana na wahalifu au kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

Akizungumza katika hafla ya kumuaga aliyekuwa kamanda wa mkoa, Suzan Kaganda na kumkaribisha Issa, Mwananzila alisema ni aibu kwa askari kushirikiana na wahalifu au kujihusisha na uhalifu.

Alisema kama tuhuma hizo zitatokea, zitalishushia hadhi Jeshi la Polisi na kuwakatisha tamaa wananchi, hivyo kumtaka kamanda mpya kuhakikisha askari wanakuwa mfano mwema kwa jamii.

Mkuu huyo wa mkoa alisema iwapo askari atagundulika kushirikiana na wahalifu au kujihusisha na uhalifu, hatua za kinidhamu zichukuliwe haraka pasipo kuchelewa.

Kwa upande wake, Kamanda Issa alisema ni vizuri ukawepo ushirikiano miongoni mwa vyombo vya dola katika kukabiliana na uhalifu.

“Kama tutashirikiana na kamati ya ulinzi na usalama tutaweza kupambana na uhalifu katika mkoa wetu,” alisema.

Naye Kaganda alilitaka jeshi hilo kuwa na malengo katika mipango ya kukabiliana na uhalifu.

Miezi michache iliyopita uligundulika upotevu wa bunduki katika ghala la kuhifadhia silaha ambazo baadhi zilikamatwa maeneo mbalimbali nchini. 


Haijulikani silaha hizo zilitokaje, ingawa baadhi ya askari walikamatwa na kufunguliwa mashtaka, huku wengine wakilalamika kuwa waliokamatwa hawakuhusika.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: