BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF) WAIPIGA JEKI HOSPITALI YA RUFAA YA MJI WA BABATI MANYARA MASHUKA 100.

Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela (kulia) akipokea moja kati ya msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kutumiwa na wagonjwa wa hospitali ya mji wa Babati (Mrara) anayemkabidhi ni meneja wa NHIF Mkoani humo, Isaya Shekifu.Picha Zote na Joseph Lyimo, MANYARA.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kutumiwa na wagonjwa wa hospitali ya mji wa Babati (Mrara), kushoto ni meneja wa NHIF mkoani humo, Isaya Shekifu na kulia ni Ofisa ushirika wa halmashauri ya mji huo Keneth Shemdoe. 

Baadhi ya wakazi wa mji wa Babati Mkoa wa Manyara, wakishuhudia Mkuu wa Wilaya ya Babati Crispin Meela akikabidhiwa msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoani humo, Isaya Shekifu kwa ajili ya hospitali ya mji huo (Mrara) ambayo inakabiliwa na upungufu wa mashuka ya kujifunikia wagonjwa wanaolazwa.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu akizungumza mara baada ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Babati Crispin Meela mashuka 100 waliyotoa msaada kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara), ambayo inakabiliwa na upungufu wa mashuka kwa wagonjwa. 

Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela (kulia) akipokea msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kutumiwa na wagonjwa wa hospitali ya mji wa Babati (Mrara) anayemkabidhi ni meneja wa NHIF Mkoani Manyara, Isaya Shekifu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: