BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATOTO WACHANGA 13 WAZALIWA MKESHA WA KRISMASI MOROGORO.


Watoto wachanga mara baada ya kuzawali katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro katika mkesha wa krismasi ambapo akinamama 13 walijifungua watoto hao. Picha na Juma Mtanda.

Juma Mtanda, Morogoro.

Jumla ya watoto wachanga 13 wakiwemo wa kiume sita na kike saba wamezaliwa baada ya wazazi wao kujifungua kwa njia ya kawaida na upasuaji katika mkesha wa sikukuu ya krisimasi katika kituo cha afya cha Mafiga na Hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro.

wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti mjini hapa, wauguzi wa zamu wa kituo cha afya Mafiga na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro walieleza kuwa akinamama 13 wamefanikiwa kupata watoto wachanga 13 baada ya kujifungua katika mkesha wa sikukuu ya krisimasi kwa mwaka 2015.

Muuguzi wa zamu hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro, Flora Lyimo alieleza kuwa katika hospitali hiyo wamezaliwa watoto wachanga saba kati yao wakiume watatu na kike wanne huku mwanamke mmoja akifungua kwa njia ya upasuaji na wengine sita wakijifungua kwa njia ya kawaida.

Lyimo alimtaja mwanamke aliyejifungua kwa njia ya upasuaji kuwa ni Shamila Abdallah (22) mkazi wa Mtawala kwa kujifungua mtoto wa kike.

Kwa upande wa muuguzi wa zamu wa kituo cha afya cha MafigaAlimwene Mwakilembe alisema kuwa katika mkesha huo wamezawaliwa watoto sita, watatu wakiwa wa kiume na kike watatu na wote wamejifungua kwa njia ya kawaida.Chanzo:MTNDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: