BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIVUKO CHA MV KILOMBERO II KUFANYIWA MAJARIBIO BAADA YA MATENGENEZO NA UKARABATI.

Juma Mtanda, Mwananchi
news@thecitizen.co.tz

Kilombero.Kivuko cha MV Kilombero ambacho kilipinduka januari 27 mwaka huu kutokana na dhuruba kali la upepo ulioambatana mavua kubwa kinatarajia kufanyiwa majaribio kati ya leo (jumapili) na kesho (jumatatu) baada ya kumalizika kwa kazi ya matengenezo na ukarabati uliodumu kwa zaidi ya siku 10 na mafundi wahandisi mkoani Morogoro.

Akizungumza na gazeti hili mmoja wa wahandisi kwa njia ya simu jana Mkuu wa Kivuko Kilombero, Fadhil Haroub alieleza kuwa kivuko cha MV Kilombero II huenda jumapili ama tatu kikafanyiwa majaribio ya kwanza tangu kipate ajali na kupinduka na kusababisha hasara mbalimbali.

Mafundi wahandisi wanaendelea na kazi ndogo zilizobakia za ukarabati na matengenezo.

Mhandisi Haroub alieleza kuwa kivuko hicho kinafanyiwa ukarabati na matengenezo usiku na mchana na mafundi wahanidisi wa kampuni ya Songoro Marine Transport ya jijini Mwanza baada ya kuopolewa rasmi februari 9 mwaka huu na kampuni ya M. Divers Ltd ya Dar es Salaam.

“Kampuni ya Songoro Marine Transport wao kazi yao kubwa ni kukarabati vivuko na meli na kiukweli nimeona kasi yao ya ukarabati na matengenezo ni kubwa kwani nina imani kati ya kesho (leo) au keshokutwa (kesho) kivuko kinaweza kikaingia majini kwa ajili ya majaribio.”alisema mhandisi
Haroub.

Ukarabati huo ni pamoja na matengenezo ya kujenga vibanda, paa na viti vya kupumzikia abiria, kurejesha milango ya kutokea abiria na magari na kupiga rangi.

Kazi nyingine ni kuifanyia matengenezo madogomadogo ya injini ya kushoto wakati injini ya kulia yenyewe ikiwa imeng’olewa na kuwekwa injini nyingine iliyokuwa ya akiba katika kivuko cha Luhuhu Songea kufuatia injini hiyo ya MV Kilombero II kuingia maji ndani ya injini baada ya kupinduka.

Mkazi wa Kilombero Halid Abeid akizungumza ka nja ya simu na mwandishi wa habari hii alisema,kwanza anaipongeza serikali kwa juhudi liyofanya mpaka sasa, na kuongeza kuwa endapo kivuko kitaanza kutumika inatakiwa kukuangalia kwa jicho la pekee na kukifanyia matengenezo ya kila mara ili kuepuka madhara kama yoliyotokea.

Abeid alisemani vyema serikali kupitia wizara ya ujenzi ikafanya ujenzi wa haraka wa daraja ili liweze kutumiaka na kuepuka ajali za mara kwa mara zinazitokea katika mto huo Kilombero.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: