BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKURUGENZI ALIYETAFUNA FEDHA ZA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA ASIMAMISHWA KAZI NA WAZIRI.

Kasi ya utumbuaji majipu katika wizara mbalimbali nchini imepamba moto baada Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Stephen Kasubi.

Kusimamishwa kazi kwa kigogo huyo kumetokana na kuwepo kwa taarifa za kampuni kupata hasara ya zaidi ya Sh. milioni 700.

Mbarawa alisema serikali ilibaini wizi huo kupitia mtandao na wafanyakazi wa ATCL kwa kushirikiana na kampuni ya Salama World Travel iliyoko katika Visiwa vya Comoro.

Akizungumza na waandishi wa habari, Profesa Mbarawa alisema: Kutokana na upotevu huo, serikali imechukua hatua thabiti ikiwamo kumsimamisha kazi Kasubi, ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi cha polisi kitengo cha usalama mtandaoni, ili kubaini mtandao mzima uliohusika.”

Alisema kwa utaratibu wa kawaida wa kampuni hiyo, wakala hupewa ruhusa ya kuuza tiketi za ndege zenye gharama ya Sh. milioni 15 tu na pale anapomaliza huzirudisha fedha kwenye kampuni kisha kupewa tiketi zingine za kiasi kama hicho.

Waziri alisema Agosti 13, mwaka jana, wakala huyo aliingiziwa tiketi kwenye mtandao zenye thamani ya sh. milioni 121 badala ya tiketi za Sh. million 15, ambazo zinatakiwa.

Aidha, Septemba 9, mwaka jana, aliingiziwa Sh. milioni 122, huku Oktoba 29 tena akiingiziwa tiketi za Sh. Milioni 81 na Novemba 27 tiketi za Sh. milioni 60, Desemba 13 za Sh. milioni 121 na Januari 10, mwaka huu, akaingiziwa tena tiketi za Sh. milioni 121.

“Siku mbili zilizopita nilifanikiwa kukutana na menejimenti ya ATCL na kubaini upungufu mwingi hivyo kuamua kuuafanyia kazi kwa kuhakikisha kampuni hii inarudi,” alisema Prof. Mbarawa.

Kutokana na ubadhirifu huo, alisema serikali imemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wa shirika hilo, ili kubaini kama fedha za uuzaji wa tiketi zinarudishwa kama inavyotakiwa.CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: