BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

"SIWEZI KUIPONGEZA KLABU YA SIMBA KWA KUONGOZA LIGI KUU TANZANIA BARA".


Na Baraka Mbolembole
Siwezi kuipongeza Simba SC kwa kuwa wamefanikiwa kuongoza ligi kuu kwa mara ya kwanza baada ya kusubiri kwa miaka mitatu mfululizo. 


Pia nitashangazwa na klabu za Yanga SC, Azam FC na Mtibwa Sugar ikiwa ‘Wekundu wa Msimbazi’ watashinda ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu.

Ni rahisi sana kwa Leicester City kushinda ubingwa wake wa kwanza wa ligi kuu England msimu, inawezekana Atletico Madrid ikashinda taji la pili la La Liga ndani ya misimu mitatu mbele ya FC Barcelona na Real, kama ambavyo SS Napoli haiwezi kushinda taji la Serie A msimu huu na ndivyo itakavyokuwa kwa timu ya Simba katika ligi kuu ya Vodacom msimu huu.

Simba haiwezi kushinda VPL licha ya kufanikiwa kushinda michezo 6 mfululizo iliyopita na kufika kileleni mwa msimamo ikitoka nafasi ya nne.

SIMBA SC
Simba wanachelea kila dakika hivi sasa, lakini wanaweza kuzishinda Yanga na Mbeya City katika michezo miwili iliyo mbele yao? Kama watashinda hapa wanaweza kufanya lolote kwa ‘kudra za Mwenyezi Mungu’

Kuongoza ligi baada ya miaka mitatu ni hatua lakini kw a timu bingwa mara 19 kihistoria si kitu cha kujivunia sana kwani ni nyakati hizi timu mpya kama Mbeya City zimewahi kufanya hivyo.

Umbo zuri la kiuchezaji wanaloingia nalo katika gemu ya ‘Dar es Salaam-Pacha’ ni dalili ya matumaini mapya lakini wanakwenda kucheza na moja ya timu ngumu kufungika ambayo tayari ilishawafunga 2-0 katika mchezo wa kwanza.

Simba wanaonekana kuchezavizuri hivi sasa lakini wamecheza na timu gani za kutisha kama Yanga na City? Wakifungwa na Yanga mbaya upande wao, na itamaanisha mchezo wa mbele dhii ya City utakuwa mgumu zaidi upande wao.

Simba wapo kileleni ikiwa na michezo 19 kwa tofauti ya pointi mbili na Yanga yenye michezo 18 katika nafasi ya pili na tofauti ya pointi tatu dhidi ya Azam FC iliyo nafasi ya tatu. Hakika wako juu lakini tawi walilopo linakwenda kuvunjika na huenda wakapotea kabisa ‘TOP 2’ kwa mara ya nne mfululizo.

Wametumia nguvu na maarifa mengi kufika walipo sasa, ila watajiangusha wenyewe kwa mara nyingine kama walivyoshindwa Napoli siku mbili zilizopita kwa kushindwa kupata walau sare tu dhidi ya Juventus ambayo ilianza msimu vibaya lakini sasa wapo kileleni kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya waliokuwa viongozi wa muda mrefu timu ya Napoli.

Kwa sasa Simba inashindana na Yanga na Azam katika mbio za ubingwa na ili waendelee kubaki juu wanapaswa kushinda gemu zao, tena zile zinazowahusu wapinzani wao hao kuwa kipaumbele.

Simba ya sasa haina uwezo wa kuishinda Yanga hii, lakini wanaweza kutimiza matarajio yasiyotarajiwa kama Leicester inavyokimbilia ubingwa wa EPL msimu huu. Simba kwa sasa haina mchezaji wa bahati ambaye anaweza kuwapa goli la ushindi kali kama lile la Machi 8, 2015 katika mechi iliyokuwa ngumu sana upande wao.

YANGA SC.

Iko nyuma kwa alama mbili dhidi ya Simba. Kitendo cha kuiwakilisha nchi katika michuano ya klabu bingwa kimetumiwa kama faida kubwa kwa Simba. Ratiba yao ni ngumu sana, watacheza na Simba siku ya Jumamosi ijayo kisha Azam FC, Machi 5.

Kitendo cha kukubali kupoteza mechi dhidi ya Simba kitafungua tofauti ya pointi 5 kati yao na Simba. Licha ya kwamba wana mchezo mmoja mkononi ( dhidi ya Mtibwa) Yanga watajiondoa wao wenyewe katika mbio za ubingwa na inawezekana kusogezwa mbele kwa mechi yao na Mtibwa ikawa afadhali kwani wasingeweza kushinda gemu zote tatu-Yanga v Mtibwa- Yanga v Simba-Azam v Yanga.

Njia pekee ya mabingwa hao watetezi kuendelea kuendelea kubaki katika njia waliyoanza nayo msimu ni kuifunga tu Simba ili kurudi kileleni, vinginevyo wataanza kupigwa presha wakati huu ligi ikizidi kuwa ngumu kuliko vile ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza.

Ni kweli, Yanga ilipoteza mchezo dhidi ya Coastal kwa magoli 2-0 na wakalazishwa sare ya 2-2 na Tanzania Prisons lakini matokeo hayo yalitokea katika michezo ya mzunguko wa 16 na 17 kwa maana nyingine hawapaswi kupoteza mwelekeo wao sahihi wa kiuchezaji na jinsi ya kuhakikisha wanapata alama 3 katika michezo migumu.

Walicheza vibaya dhidi ya Coastal wakiwa bila Nahodha, Nadir Haroub na kiungo, Mzimbabwe, Thaban Kamusoko na hawatakuwa na Kelvin Yondan katika michezo muhimu zaidi dhidi ya Simba na Azam.

Hiyo ni dalili mbaya kwao lakini bado wanaweza kuendelea kufunga magoli ya kutosha kutokana na makali ya safu yao ya mashambulizi ambayo imefunga katika 16 kati ya 18 ya VPL hadi sasa huku wakifanya hivyo mara mbili dhidi ya Simba na mara moja dhidi ya Azam FC.

AZAM FC
Wamechapwa kwa mara ya kwanza msimu huu katika uwanja ule ule ambao Yanga walipoteza mechi yao ya kwanza kwa msimu, mguu ule ule uliowamaliza Yanga ndiyo uliowanyonga na wao, ni timu ile ile ya Coastal ‘nyanya’ ndiyo iliyomfanya kocha wao Stewart Hall kuwakwepa wanahabari baada ya mchezo kumalizika.

Daah! Azam nao wanakwenda katik a ratiba ngumu ‘kimuonekano’. Kipigo cha Coastal kimekuja wakati mbaya licha ya kwamba watakuwa na michezo miwili ya viporo.

Wamepoteza mechi ya kwanza katika gemu ya 17 hawapaswi kuweweseka zaidi ya kwenda Mbeya kujaribu kuishinda Mbeya City yenye kocha mpya Mmalawi, Kinnah Phiri ambaye tayari ameanza VPL na ushindi wa 5-1 dhidi ya Toto Africans siku ya Jumamosi iliyopita.

Azam wapo imara na wanaweza kushinda dhidi ya City kisha Yanga lakini si kwa kiwango wanachoonyesha sasa. Wana kazi kubwa ila ubingwa uko mikononi mwao.

MTIBWA SUGAR
Ikiwa imecheza mechi 17 mbili pungufu ya zile za Simba, timu hiyo ya Turiani, Morogoro tayari imepitwa pointi 13 na Simba. Timu ambayo ilikuwa ‘bega kwa bega’ na timu za Yanga na Azam hadi mwezi Januari mwaka huu imeanza kudhohofu na kupoteza makali.

Nitashangaa hakika kama Simba watakuwa mabingwa wa VPL msimu huu na si Mtibwb. 


Top5 si faida kwao ila itawalindia heshima. Hawa wameshindwa vita mapema kama ilivyo kawaida yao, wana msemo ‘ Tutarudi msimu ujao’ msimu gani huo?
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: