Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Habari kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo, Richard Kayombo. Picha ya Maktaba
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewabadilishia vituo vya kazi watumishi zaidi ya 100 ili kuimarisha uwajibikaji na kuongeza ufanisi.
Hatua hiyo inakuja baada ya hivi karibuni watendaji wakuu wa mamlaka hiyo kupata ‘mtikisiko’ kutokana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Mmoja wa watendaji waliopata ‘mtikisiko’ ni Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade ambaye amesimamishwa kazi na Rais John Magufuli kupisha uchunguzi wa utoroshaji wa makontena 300.
Wiki mbili baadaye, aliyekuwa kaimu wa nafasi hiyo, Dk Philip Mpango aliwasimamisha kazi watumishi 37 kutokana na sakata hilo.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Habari kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo, Richard Kayombo alisema leo kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida.
“Huwa tunafanya hivi mara kwa mara. Lengo ni kuwabadilishia vituo wale waliofanya kazi sehemu moja kwa muda mrefu, kuziba nafasi zilizoachwa wazi na wastaafu, waliopandishwa vyeo au waliofariki dunia pamoja na kubadili mazingira,” alisema.
Alisema uhamisho huo una nia ya kuongeza uzoefu miongoni mwa watendaji wa mamlaka hiyo na utafanyika mwingine pale itakapoonekana kuna mahitaji hayo.MWANANCHI DIGITAL
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ WAFANYAKAZI 100 WA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) WAHAMISHWA VITUO VYA KAZI
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment