BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KUSHUKA KWA DARAJA KWA KLABU YA BURKINA FC KWAWASONONESHA WADAU WA SOKA MOROGORO.

Juma Mtanda, Mwananchi.
Wadau wa soka na mashabiki wa klabu ya Burkina FC ya Morogoro walipandwa na jazba baada ya timu hiyo kushuka daraja katika ligi daraja la kwanza Tanzania bara kufuatia kupokea kipigo cha bao 3-2 na JKT Mlale ya Songea katika mchezo wa mwisho uliofanyika uwanja wa jamhuri Morogoro jana.

Kutokana na kipigo hicho, Burkina imeshuka daraja la kwanza na kuingia daraja la pili baada ya kudumu ligi daraja la kwanza kwa miaka tisa mfululizo wakijukama kama kisiki cha mpingo.

Jazba hizo zilitokana na madai ya wadau wa soka na mashabiki wakiwatuhumu viongozi wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Morogoro (MRFA) kushindwa kuzisaidia klabu katika maandalizi mbalimbali za michezo yao.

Mpaka sasa timu mbili zilizokuwa zinashiriki ligi daraja tayari zimeshuka daraja pamoja Mkamba Rangers FC na Burkina FC ambazo sasa zitacheza ligi daraja la pili ngazi ya taifa.

Timu nyingine ni klabu ya Polisi Moro SC ambayo imeshuka kutoka ligi kuu ya vodacom na kubakia ligi daraja la kwanza huku ikiwa imefanya vibaya katika michezo ya ligi hiyo kusaka nafasi ya kurejea tena ligi kuu ya vodacom msimu ujao.

Timu iliyopanda daraja na kurejea ligi kuu ni Ruvu Shooting katika kundi hilo.

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Polisi Moro SC, Ally Moshi aliungana na mashibiki waliohudhuria mchezo huo kwa kueleza kuwa ameshangazwa na kitendo cha Burkina FC kufungwa bao 3-1 kipindi cha kwanza katika uwanja wake wa nyumbani tofauti na timu hizo zinapoenda kucheza michezo katika viwanja vya ugenini.

“Nimeshangazwa kuona timu mwenyeji eti kipindi cha kwanza tu anafungwa bao 3-1 tena katika uwanja wake wa nyumbani ?...inachosha na aina ya viongozi wanaongoza mchezo wa soka ngazi ya mkoa”.alisikika Moshi huku akiondoka uwanjani hapo.

Kauri nyingine zilisika kutoka kwa mashabiki muda mchache kabla ya kumalizika mchezo huo zikimkumbuka aliyewahi kuwa katibu mkuu chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) marehemu, Salum Mwintanga kwa uongozi wake wa kutukuka na kuzisaidia timu za mkoa huo.

“Tunakukumbuka kwa heri Katibu wetu Mwintanga kwani asingeweza kuona timu kama Polisi Moro SC, Mkamba Rangers na Burkina FC zinashuka ovyo hovyo kwa hatua kubwa zilizofikia zaidi ya kuongeza nguvu kwenda ligi kuu Tanzania bara inayodhaminiwa na vodacom.”ilisikika sauti ya mmoja wa mashabiki hao akilalama.

Mshambuliaji wa Burkina FC, Victor Mswaki alieleza kuwa timu ya Burkina ni timu mzuri isipokuwa imekosa matunzo na uangalizi wa katibu kutoka kwa viongozi wa chama cha soka mkoa wa Morogoro na ndiyo sababu ya wao kushuka daraja na timu nyingine kama Polisi Moro SC na Mkaamba Rangers.

“Ni jambo lililowazi mwandishi, chama cha soka hakina msaada kwa timu hasa zinazochenga michezo ngazi ya taifa kama ligi daraja la pili, daraja la kwanza hadi ligi kuu tofauti na Mtibwa Sugar ambayo inajitegemea kwa kila jambo pengine haiathiriki na hali kama timu za Polisi Moro, Mkamba Rangers na Burkina.”alisema Mswaki.

Mswaki alisema kuwa katika mchezo wao dhidi ya Simba SC wa FA Cup 2016 hakuweza kuona kiongozi wa MRFA wala wa serikali ngazi zote ilhali Burkina ilikuwa ikiwakilisha mkoa katika mashindano hayo.

Katika mchezo huo Burkina FC ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuruhusu nyavu zake kutikiswa baada ya kufungwa mabao ya haraka haraka katika dakika ya 16 lilipachikwa wavuni na Edward Songo akipokea pasi ya Richard Mwandiga.

Dakika ya 20 na 37 mshambuliaji, Richard Mwandiga alishindilia msumari kwa kufunga bao hizo.

Mabao ya Burkina yalifungwa na Jonathan Kishimba (Jaja) dakika ya 22 huku Victor Mswaki akifunga la pili kwa kishwa akiunganisha majaro ya Mgandila Shabaani na kufanya mchezo huo umalizike kwa JKT Mlale kuibuka na ushindi wa bao 3-2.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: