WAKURUGENZI WANNE WA BOHARI YA DAWA (MSD) WASIMAMISHWA KAZI KWA UBADILIFU WA SH 1.5 BILIONI NA WAZIRI.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi leo wakurugenzi wanne wa Bohari ya Dawa (MSD) kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.5.
Mwalimu amewataja wakurugenzi hao kuwa ni Mkurugenzi wa manunuzi Heri Mchunga, Mkurugenzi wa Huduma za Kanda na Wateja Cosmas Mwaitani, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango Joseph Tesha, pamoja na Mkurugenzi wa ugavi Missanga Musa.
Waziri pia amesema ameshamwagiza Mkuu wa Bodi ya Bohari ya Dawa kuwaandikia barua za kusimamishwa kazi wakurugenzi hao ili uchunguzi dhidi yao uweze kuanza mara moja. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment