BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKWASSA AJAZA WACHEZAJI WA YANGA SC TIMU YA TAIFA YA TANZANIA (TAIFA STARS) DHIDI YA CHAD MICHEZO YA KUFUZU AFCON

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager, Charles Boniface Mkwasa leo ametangza kikosi cha wa wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Chad, Machi 23, 2016 mjini Djamena.

Akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza kikosi hicho, Mkwasa amewaomba wachezaji aliowaita katika kikosi hicho, kujiweka fit katika mazoezi wanayoyafanya katika vilabu vyao, kwani hakutakua na muda wa kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo wa ugenini.

“Ligi Kuu ya Vodacom, michuano ya CAF (CL, CC) inachezwa wikiendi ya tarehe 18-20 Machi, hivyo wachezaji wote watakua na majukumu katiak timu zao, muda wa kufanya mazoezi kwa pamoja kwa ajili ya mchezo huo hautakuwepo, ndio maana nasisitiza wachezaji niliowachagua wahakikishe wanajilinda wenyewe kwa kuwa fit wanapokuja kwenye safari ya mchezo huo wa machi 23, 2016” alisema Mkwasa

Wachezaji walioitwa Taifa Stars ni magolikipa Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustapha (Young Africans) na Shaban Kado (Mwadui FC), walinzi ni Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani (Young Africans), Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam FC) na Mohamed Hussein (Simba SC).

Viungo Himdi Mao (Azam FC), Ismail Juma (JKU), Jonas Mkude, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Farid Mussa (Azam FC), Deus Kaseke (Young Africans).

Washambuliaji ni Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), John Bocco (Azam FC), Elias Maguri (Stand United), Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na Ibrahim Hajibu (Simba SC).
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: