Mshambuliaji wa klabu ya Yanga SC, Amis Tamwe amepachika mabao mawili kati ya matano dhidi ya African Sport ya Tanga katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuufanya ushindi huo kuiengua Simba SC ilikuwa ikiongoza ligi kwa muda.Tamwe amefunga mabao hao baada ya kupokea pasi ya Kamusoko aliempenyezea pasi ya mwisho na kufunga bao la pili wakati bao lake la kwanza kwa Tambwe dakika ya 51 baada ya pasi ya Haroun Niyonzima na kukokota mpira na kujaza kimiani.
Mabao mengine ya Yanga SC yalizamishwa nyavuni na Matheo Antony aliyefungwa kwa kichwa kiustadi kufuatia kazi krosi maridadi ya Mwinyi Haji huku mshambuliaji Donald Ngoma akifunga dakika ya 38 kwa pasi ya Juma Abdul wakati mlinizi Kelvin Yondani akifungua kalamu ya mabao kwa kufunga dakika ya 32 katika mchezo huo uliowafanya African Sport ya Tanga ikubali kutandikwa bao 5-0.

0 comments:
Post a Comment