Klabu ya Yanga imefanikiwa kuilaza APR ya Rwanda katika mchezo wa klabu bingwa ugenini baada ya Juma Abdul na Kamusoko Thaban kufunga mabao kila kipindi huku wenyeji wakipata bao moja katika ushindi wa bao 2-1.Juma Abdul alifunga bao la kwanza katika kipindi cha kwanza kwa njia ya adhabu ndogo iliyoenda moja kwa moja wavuni kabla Kamusoko Thaban kufunga bao la pili kipindi cha pili na APR akipata bao la kufutia machozi.
Kutokana na ushindi huo Yanga wamejiweka katika mazingira mazuri ya kuvuka hatua inayofuata baada ya ushindi huu ugenini na endapo itavuka hatua hiyo Yanga itakumbana na National Al Ahly ya Misri au Recreativo Libolo Angola.

0 comments:
Post a Comment