Dany Lyanga wa Simba (10), akijaribu kufunga bao, huku akiwa amezungwa na mabeki wa Coastal Union ya Tanga.
WEKUNDU wa Msimbazi wamepotea. Ndilo neno
rahisi unaloweza kulisema, baada ya wavaa jezi hao nyekundu na nyeupe
kutupiliwa mbali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho (FA), wakikubali
kipigo cha mabao 2-1 kutoka Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam jana.
Matokeo hayo ya hatua ya robo fainali, yana maana kwamba, sasa Simba haitashiriki michuano ya kimataifa mwakani, labda itwae ubingwa wa Ligi Kuu Bara unaowaniwa kwa karibu na Yanga na Azam FC.
Kwa mwaka wa nne mfululizo, Simba haijawahi kutwaa la Ligi Kuu Bara wala kumaliza katika nafasi ya pili, hivyo kukosa fursa ya kushiriki michuano ya Afrika.
Bingwa wa michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho ndiye atakayevaa ‘viatu’ vya nchi kucheza michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) – Kombe Shirikisho.
Katika mechi hiyo, Coastal inayopigania kubaki Ligi Kuu Bara ikiburuza mkia, ilicheza kama siyo vile siyo timu ‘inayogawa’ kwenye mechi za ligi na kuwashangaza Simba.
Simba waliyoifunga Coastal Union mara mbili – nyumbani na ugenini kwenye mechi za ligi, ilijikuta nyavu zake zikitiswa dakika 19 baada ya kuanza kipindi cha kwanza kupitia kwa Yossouph Sabo, ambaye kiki yake ya mpira uliokufa kwenda moja kwa moja kwenye kamba za Msimbazi na kudumu hadi mapumziko.
Haraka haraka baada ya kuanza kipindi cha pili, Simba walisawazisha bao hilo kupitia kwa Hamis Kiiza aliyeingia akitoka benchi kuchukua nafasi ya Said Ndemla.
Kiiza aliutumbukiza wavuni mpira kwa kichwa akimalizia krosi ya Ibrahim Ajib.
Mambo yalizidi kuwanyookea Coastal Union waliojihakikishia ushindi dakika tano kabla ya filimbi ya mwisho kwa kufunga bao la pili.
Bao hilo lililopeleka majonzi Msimbazi liliwekwa kwenye kamba na Sabo kwa mkwaju wa penalty baada ya Novatus Lufunga kumchezea vibaya, Ally Shiboli na mwamuzi Alex Mahagi kutoka Mwanza kupuliza filimbi.
Kwa ushindi huo sasa Coastal Union inaungana na Yanga, Azam, na Mwadui kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / michezo /
slider
/ SIMBA SC NAMNA ILIVYOTUMBULIWA JIPU NA COASTAL UNION, ROBO FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHI (FA).
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment