BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VYOMBO VYA HABARI VYAAMBIWA KUIGA MFUMO BORA WA UENDESHAJI WA KAMPUNI YA MWANANCHI COMMUNICATION LTD


Mkuu wa Uhusiano wa kampuni ya TBL, Emma Urio akimkabidhi Tuzo ya Mazingira mwandishi wa gazeti la The Citzen, Sauli Gilliard wakati wa utoaji wa Tuzo za Umahili za EJAT. Picha zote na Said Khamis.

Mwanza.
Vyombo vya habari vimeshauriwa kuiga mfumo wa uendeshaji kampuni ya Mwananchi Communications Limited ili kukidhi mahitaji ya tasnia na kuepuka migongano.

Makamu mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile ametoa ushauri huo leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mjini hapa.

Balile amesema mfumo wa Mwananchi unatoa uhuru kwa vyombo vya habari vya kampuni hiyo, inayomiliki magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, kufanya kazi kwa uhuru bila ya kuingiliwa na viongozi. 


“Wahariri wa Mwananchi wako huru kwa sababu wanafanya kazi zao bila ya kuingiliwa na CEO (mkurugenzi mkuu) wao ambaye ana jukumu la kushughulikia utawala jwa ujumla na masuala ya biashara, lakini newsroom Chumba cha habari) inabaki kwa wahariri na waandishi wao ili wafanye kazi zao kitaaluma zaidi,” amesema Balile.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: