MAJI YA SHINGO ! MFANYABIASHARA ASALIMISHA SUKARI YA TANI 33 KWA MKUU WA MKOA ARUSHA.
Arusha. Wakati watu tisa wameshakamatwa hadi sasa katika msako wa wanaoficha sukari, mfanyabiashara mmoja kigogo mjini hapa amesalimisha tani 33 kwa mkuu wa mkoa.
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa limekuwa likifanya msako huo ambao umebaini kuwa wafanyabiashara wote wanaouza sukari tofauti na bei elekezi.
Mfanyabiashara huyo, Romanus Macha asalimisha tani 33 za sukari zilizokuwa kwenye mifuko ya kilogramu 50.
Macha aliiambia kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya iliyokuwa kwenye msako huo kuwa ameamua kusalimisha sukari hiyo ili kutii agizo la Serikali kuhusu kupanga bei elekezi ya Sukari .
Alisema sukari hiyo ilifikia jana asubuhi na alishaitolea taarifa kwa mkuu wa mkoa na wa wilaya kuwa ana sukari
"Utaratibu ulioko sasa ni kwamba kama kuna sukari unatakiwa utoe taarifa kwa mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya, ili akupangie jinsi ya kuuza.
Nilimsikiliza Rais wakati akiagiza hivyo na ndivyo nilivyofanya kabla ya sukari kuwasili," alisema Romanus.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment