BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ARGENTINA YATUMBULIWA TENA NA CHILE KATIKA FAINALI YA KOMBE LA COPA AMERIKA KWA BAO 4-2 NA KUKOSA UBINGWA.

Timu ya taifa ya Argentina imeendeleza unyonge mbele ya taifa la Chile baada ya kufungwa katika fainali ya michuano ya Copa America 2016 kwa kucharazwa bao 4-2 zilziotokana na mikwaju ya penalti katika uwanja wa MetLife jiji la New Jersey Marekani alfaji ya Juni 27 mwaka huu.

Mashabiki wa soka la bara la America walishuhudia fainali hiyo ikiwakutanisha wababe hao huku Chile ikionekana mbabe mbele ya
Argentina kwa kukutana katika hatua ya fainali ya michuano hiyo, baada ya sare tasa ya 0-0 ndani ya dakika 120.


Hii ni fainali ya tatu mfululizo timu ya taifa ya Argentina ikikosa Ubingwa ambapo ilikosa ubingwa wa Kombe la dunia 2014 dhidi ya Ujerumani, ikarudia tena kukosa taji la Copa America 2015 katika hatua ya fainali na Chile huku alfajili ya leo June 27 ikipoteza tena mchezo wa fainali kwa mara ya pili mfululizo kwa Chile.

VIDEO YA MCHEZO WA FAINALI KATI YA ARGENTINA NA CHINI
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment