BODABODA 40 WAKAMATWA NA ASKARI KWA KOSA LA KUTAKA KUJIUA.
Dar es Salaam. Wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatoa agizo la kukamatwa abiria wanaopanda bodaboda bila kuvaa kofia ngumu ili washtakiwe kwa kutaka kujiua, ilionekana kama mzaha lakini watu wameanza kuonja shubiri yake.
Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke inawashikilia zaidi ya watu 40 kwa tuhuma za kutovaa kofia ngumu wakati wakisafiri kwa pikipiki.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Gilles Muroto aliliambia gazeti hili jana kuwa, watuhumiwa hao wakiwamo waendesha bodaboda, walikamatwa kwa nyakati tofauti tangu msako uanze juzi.
“Ukikuta dereva hana kofia mbili mtafute mwingine mwenye kofia au tafuta usafiri mwingine unaoona unakufaa,” alisema Muroto.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment