KATIBU MKUU OFISI YA RAIS UTUMISHI AMPONGEZA MKUU WA MKOA WA MBEYA WA KUTENGA SIKU YA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI
Katibu Mkuu ofisi ya Rais Dr Ndumbaro kushoto akisalimiana na mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla mkoa huo.
Katibu Mkuu ofisi ya Rais Dr Ndumbaro ameupongeza utaratibu aliouweka Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos G Makalla wa kutenga kila siku ya alhamis ya mwanzo wa mwezi na wiki ya mwisho wa mwezi kuwa siku ya kusikiliza Kero za wananchi.
Aidha ameweka utaratibu wa wakuu wote wa wilaya kila wiki siku ya Alhamis kuwa siku ya kusikiliza kero za wananchi.
Amesema hayo leo alipokuwa katika ziara za kusikiliza Kero za watumishi katika Mkoa wa Mbeya na kusisitiza kuwa ofisi ya Rais utumishi imetoa maelekezo ya kusikiliza Kero za watumishi na wananchi na ametaka mikoa mingine kuiga utaratibu wa mkoa wa Mbeya ili kushughulikia kero za wananchi na watumishi kwa haraka.
Mkuu wa mkoa amehaidi kuendeleza utamaduni huu na wananchi wa Mkoa wa Mbeya wameupokea kwa furaha
0 comments:
Post a Comment