BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KILOSA YATENGA KIASI CHA SH80 MIL KWA AJILI YA KUNUNUA PEMBEJEO ZA KILIMO KATIKA MSIMU UJAO.

Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro, John Henjewele akimsikiliza Kiongozi wa kusambaza tekinolojia za mradi wa Simlesa Tanzania (ARI-Ilonga) Bashir Kikoko juni 22 mwaka huu wakati akizungumza jambo katika mashamba darasa la mkazi wa kijiji cha Mhenda tarafa ya Ulanya wilayani humo, Bonasi Mbabe.PICHA/MTANDA BLOG

Juma Mtanda, Morogoro

Serikali ya wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro imetenga kiasi cha sh80 milioni kwa ajili ya kununua pembejeo za kilimo msimu ujao wa kilimo huku ikiagiza wakulima kutumia vyema utafiti unaotolewa na watalamu wa kituo cha utafiti cha kilimo cha Ilonga ili kilimo kiwe na tija na mkulima kuongeza uhakika wa chakula na kipato.

Akizungumza na wakulima zaidi ya 200 kijiji cha Mhenda tarafa ya Ulaya wilayani Kilosa, Mkuu wa wilaya hiyo, John Henjewele alisema kuwa ili kilimo kiwe na tija na kumkomboa mtanzania ipo haja kwa wakulima kutumia vyema utafiti unaofanywa na kutolewa na watafiti wa kilimo hapa nchini.

Sherehe hizo zilihusisha wakulima kutoka vijiji vya Ilakala, Nyalanda na Mhenda ikilenga kuonyesha tekinolojia mbalimbali zinazotolewa na mradi wa Simlesa na lengo kuu ikiwa kuwawezesha wakulima kuongeza uhakika wa chakula na kipato kutumia mfumo wa kilimo mseto cha mahindi na mikunde chini ya kilimo hifadhi na matumizi ya mbolea.

Henjewele alisema kuwa serikali ya wilaya hiyo katika msimu wa kilimo ujao umetenga kiasi cha sh80 milioni ili fedha hizo zitumike kununua pembejeo za kilimo ikiwa ni mpango wa kuunga mkono juhudi za watafiti wa kilimo ili kuinua kilimo nchini.

“Tayari Kilosa imepitisha bajeti ya sh80 milioni na fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kununua pembejeo za kilimo na hii ni katika kuunga juhudi za watafiti wa kilimo ambao katika kilimo cha kisasa hulazimika kutumia mbolea ikiwa ni mojawapo ya pembejeo za kilimo.”alisema Henjewele.

Kwa upande wa mmoja wa wakulima, Bonasi Mbabe alieleza kuwa endapo mkulima atafuata ushauri wa watalaamu wa utafiti wa kilimo kinamwawezesha mkulima kuongeza uhakika wa chakula na kipato baada ya kulima kilimo cha mseto cha mahindi na mikunde.

Kiongozi wa kusambaza tekinolojia za mradi wa Simlesa Tanzania (ART-Ilonga), Bashir Makoko alisema kuwa mradi wa Simlesa umelenga kutafiti na kueneza mifumo ya kilimo endelevu cha mseto wa mahindi na mikunde kwa ajili ya kuwa na uhakika wa chakula mashariki na kusini mwa afrika.

Kikoko alieleza kuwa kilimo mseto ninawawezesha wakulima kuongeza uhakika wa chakula na kipato kwa kutumia tekinolojia za kilimo cha mseto cha mahindi na mikunde ndani ya kilimo hifadhi na heka moja huvunwa kiasi cha gunia 10 hadi 15.

Nchi zilizopo kwenye mradi huo ni Ethiopia, Kenya, Tanzania, Malawi na Msumbili na upande wa Tanzania mradi huo umejikita nyanda za juu katika mikoa ya Arusha na Manyara wakati nyanda za chini ya mashariki, mikoa ya Morogoro ni wilaya za Gairo, Mvemero na Kilosa.Chanzo:MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: