BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAITI NA WAGONJWA WALAZWA CHUMBA KIMOJA KITUO CHA AFYA SHINYANGA.


Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Novemba 9 2015.

Kahama. Kaimu Mganga Mfawidhi wa Bulungwa kilichopo Halmashauri ya Ushetu, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Peter Dalali amesema wanalazimika kulaza maiti ndani ya wodi ya wagonjwa hadi asubuhi kutokana kukosekana kwa chumba cha kuhifadhia maiti.

“Tunachofanya ni kutenganisha wagonjwa na maiti kwa kutumia pazia hadi asubuhi ndugu wanapokuja kuchukua mwili wa marehemu,” alisema Dalali.

Kituo hicho cha afya kilichopandishwa hadhi kutoka zahanati bado Serikali haijakijengea chumba cha kuhifadhi maiti. “Ni vyema kabla ya kupandisha zahanati kuwa kituo cha afya iwepo miundombinu ya kutosha kwa kufuata vigezo, badala ya kuibua hofu kwa wagonjwa,” alisema Dalali.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: