BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAKUNDI LIGI DARAJA LA KWANZA YAPANGWA, POLISI MORO YAANGUKIA KUNDI LA TIMU ZA NYANDA ZA JUU KUSINI.

Kikosi cha timu ya Polisi Moro SC.

Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza makundi matatu ya timu zitakazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes msimu wa 2016/2017. 

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Agosti, mwaka huu mara baada ya kukamilisha mchakato wa usajili unaoanza Juni 15, 2016.

Makundi hayo yenye timu nane (8) kwa kila moja, yamegawanywa kwa alama ’A’, ‘B’ na ‘C’.

Katika kundi A lina timu za:
1 Abajalo ya Dar es Salaam
2 African Sports ya Tanga
3 Ashanti United ya Dar es Salaam
4 Kiluvya United ya Pwani
5 Friends Rangers ya Dar es Salaam
6 Lipuli ya Iringa
7 Mshikamano FC ya Dar es Salaam
8 Polisi Dar ya Dar es Salaam

Wakati kundi B likiwa na timu za

1 JKT Mlale ya Ruvuma
2 Coastal Union ya Tanga
3 Kimondo FC ya Mbeya
4 Kinondoni Municipal Council ya Dar es Salaam
5 Kurugenzi ya Iringa
6 Mbeya Warriors ya Mbeya
7 Njombe Mji ya Njombe
8 Polisi Morogoro ya Morogoro

Huku kundi C kukiwa na timu za
1 Alliance Schools ya Mwanza
2 Mgambo Shooting ya Tanga
3 Mvuvumwa FC ya Kigoma
4 Panone FC ya Kilimanjaro
5 Polisi Dodoma ya Dodoma
6 Polisi Mara ya Mara
7 Rhino Rangers ya Tabora
8 Singida United ya Singida
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: