BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBINU ZA KITAALAMU ZA KUANDAA LISHE BORA KWA MTOTO WA MIEZI SITA NA KUENDELEA.


Lishe ya mtoto (Butternut, gimbi, carrot na maziwa.

Lishe ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto na hili si jambo geni sana katika lishe bora ambayo imekuwa ni lazima kwa watoto wadogo sababu wanatakiwa kukua vizuri  kimwili na kiakili.

Je lishe bora ni ipi?
Lishe bora ni chakula chenye virutubisho vyote muhimu kwa kiasi na uwiano sahihi ili kuuwezesha mwili wa mtoto kupata afya bora na wataalamu wanachambua zaidi kwa kueleza kuwa lishe bora ina virutubisho aina sita ambayo ni pamoja na wanga, protein, mafuta, vitamin, madini na maji.


Je vyakula gani ambavyo ni bora ?.

Lishe bora inatakiwa kuwa na mboga za majani, matunda, protini, wanga na madini ya kutosha hizi zinapatikana kwenye vyakula aina tofauti na kuna vyakula vingine vina virutubisho vingi kwa pamoja.

Mfano wa vyakula vyenye lishe bora kwa kiwango kinachofaa ni kama mboga za majani, matunda, nafaka asilia, vyakula vya protini (mayai, maharage, nyama n.k) na vyakula vyenye mafuta yasiyohifadhiwa mwilini.

Watoto wanagawanyika katika makundi makuu mbili ambayo moja linaanza mwezi mmoja tangu kuzaliwa hadi miezi 6 na kuanzia miezi 6 na kuendelea huku makundi hayo yakitajwa kuwa ni muhimu sana kwa sababu watoto waliopo kwenye makundi hayo wanatofautiana aina za vyakula wanavyokula, na muhimu zaidi kuzingatia hilo sababu huu ndio muda muhimu zaidi katika ukuaji wa mtoto. 


Lishe ya mtoto mchanga hadi miezi 6 Inashauriwa kuwa mtoto mchanga – tangu anazaliwa hadi afikapo miezi 6 – asipewe kitu chochote zaidi ya maziwa ya mama, hii ikiwa inamaanisha hata maji ya kunywa. Maziwa ya mama yana virutubisho vyote muhimu (pamoja na maji) vinavyohitajika kwenye ukuaji mzuri wa mtoto na kumpa kinga ya magonjwa mbalimbali.

Lishe ya mtoto kuanzia miezi 6 Mtoto akishafika umri wa miezi 6, anaweza kuanza kula vyakula mbali mbali. Inashauriwa mtoto aanze kupewa vyakula mbali mbali kidogo kidogo ili apate kuzoea.


Vyakula hivi lazima viwe vimepondwa, au viwe kwenye mfumo wa uji au maji sababu mtoto anakuwa hana meno yaliyokomaa au wengine wanakuwa hawajaanza kabisa kuota meno.

Lishe ya Mama

 

Ukizungumzia mtoto hutoweza kuacha kuzungumzia mama. Mama ndiyo chanzo kikubwa cha chakula kwa mtoto tangu anazaliwa hadi anakuwa huru kula chakula cha kawaida. Kwa mwanamke mwenye umri wa kubeba ujauzito au mwenye ujauzito, ni muhimu kula vizuri ili kujenga afya ambayo ndio chanzo kikubwa cha virutubisho kwa mtoto tumboni na baada ya kuzaliwa. 


Ili kuwa na siha nzuri, vyakula vyote vinatakiwa kuwa na uwiano mzuri wa virutubisho.

Inatakiwa kuzingatiwa kuwa, vyakula vya mtoto viwe vya kuongezea lishe, lakini ni vizuri mtoto akiendelea kunyonya maziwa ya mama hadi atakapofikisha miezi 24. Maziwa ya mama ni muhimu katika kumfanya mtoto akue vizuri, hasa katika miezi 24 ya mwanzo. 


Inashauriwa kuwa, kama hakuna kikwazo – mfano: ugonjwa wa maambukizi unaoweza kumdhuru mtoto – ni vizuri mama amnyonyeshe mtoto kwa muda mrefu zaidi ya miezi sita (6).


Faida kubwa ya kunyonyesha ni kusaidia ubongo wa mtoto kukua vizuri zaidi sababu maziwa ya mama yanatoa virutubisho kwa wingi kuliko vyakula atakavyokula yeye moja kwa moja. 


Hii ni kwa sababu, tumbo la mtoto linakuwa halijazoea kusaga vyakula tofauti, hivyo maziwa ni chakula kinacholeta virutubisho vinavyotumika moja kwa moja mwilini.

Umuhimu wa lishe bora Kama ilivyoelezwa mwanzo, lishe bora ni muhimu. Zifuatazo ni baadhi ya faida apatazo mtoto anayepata lishe bora:

Kuimarisha mfumo wa kinga mwilini na kuufanya mwili kupambana kirahisi na magonjwa kama utapiamlo (kwashiorkor) na kiriba tumbo.


Kujenga siha nzuri (afya bora)
Kuleta furaha na Amani
Kusaidia ukuaji wa mwili na akili
Kuleta nguvu na kusaidia mwili kufanya kazi vizuri
Madhara ya lishe duni Kama mtoto akiwa na lishe duni, haya yatakuwa madhara yake:

Kupata magonjwa mara kwa mara sababu anakosa kinga madhubuti dhidi ya magonjwa.


Kudumaa kukua mwili na akili
Uwezekano mkubwa wa kupata ulemavu sababu mifupa inakuwa laini na haiwezi kustahimili uzito wa mwili.
Upungufu wa damu hivyo kudhoofisha afya ya mtoto
Kupata utapiamlo (Kwashiorkor)
Kupoteza maisha katika umri mdogo
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: