Na Juma Mtanda, Morogoro.
Ilichapishwa Julai 30, 2010.
SIKU chache baada ya Nomsa Mpetwane (24) mwaka 2010 kutaka kuonana na mama yake mzazi, Miriam Chimile mkazi wa kijiji cha Magole kitongoji cha Manyata mkoani Morogoro imebainika kuwa mama huyu amefarikia dunia mwaka1993 kwa ugonjwa wa kifua kikuu.
Taarifa za kifo cha Miriam Chimile zilipatikana baada ya mtoto huyo kutaka kuonana na mama yake mzazi ambapo kisa hicho kiliibuliwa na mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications, Frank Sanga ambaye kwa hivi sasa ni mhariri mkuu ambaye alikuwa nchini Afrika ya Kusini kuripoti habari za michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 zilizofanyika bara la afrika kwa mara ya kwanza.
Nomsa alionana na Sanga katika uwanja wa Soccer City ambaye Baba yake ni raia wa Afrika ya Kusini na Mama Mtanzania kupotezena naye kwa zaidi ya miaka 25 akiwa na miaka minne tu wakati walipondoka na baba yake Lebonang Christopher Mpetwane kwenda Afrika ya Kusini baada ya kumalizika kwa ubaguzi nchini humo.
Miriam Chimile akiwa na mtoto wake Masha Dyagule enzi za uhai wake.
Kutokana na hali hiyo Nomsa Mpetwane amekuwa akikosa raha ya maisha kwa kutomuona mama yake, Miriam Chimile ambaye kwa sasa ni marehemu akiwa na miaka 34.
Mwandishi wa habari hizi alifanya jitihada za kwenda katika kijiji cha Magole kipindi hicho na kufika kitongoji cha Manyata wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro na kukutana na Naomi Godwin (58) ambaye ni dada wa Miriam Chimile na kutoa simulizi za kifo cha mdogo wake huyu aliyefariki dunia mwaka 1993 na kuzikwa katika mji mdogo wa Dumila wilaya ya Kilosa.
“Mwanangu huyu unayemuulizia hapa ndipo nyumbani kwao lakini mdogo wangu huyo Miriam Chimile amefariki dunia tangu mwaka 1993 na tumemzika kwa kaka yetu kule kijiji cha Dumila.” Alisema Naomi Godwin.
Akielezea maisha ya mdogo wake Miriam na Lebonang Christopher Mpetwane maarufu kwa jina la Ndlela wakati wa mahusiano yao alisema Ndlela alikuwa na kawaida ya kumchukua mdogo wake na kwenda naye katika kambi ya wakimbizi ya Dakawa kisha kumrudisha jioni ambapo hali hiyo iliendelea na hatimaye alipata ujauzito na kuzaliwa mtoto wa kiume anayefahamika zaidi kijiji hapo kwa jina la Magaya Mpetwane aliyezaliwa mwaka 1984.
Baada ya hapo mdogo wake, Miriam Chimile alipata ujauzito wa pili na kuzaliwa mtoto wao wa kike aitwaye Nomsa mwaka 1986 ambapo wazazi wa Miriam walimwita mwanaumu (Nomsa) lakini Lebonang Mpetwane alitozwa faini ya kumpa ujauzito binti yao ambapo alitoa pesa za faini kwa kosa hilo.
Muwe huyo wakati huo alikuwa akiishi Mateteni Dakawa Centre ambako kulikuwa na kambi ya wakimbizi wa Afrika ya Kusini na mwanamke akiishi kwenye kijiji cha Magole kitongoji cha Manyata. Alieleza, Naomi Godwin.
Baada ya kuzaliwa kwa Nhanhla, alipata ujazito wa pili na kumzaa mtoto wa kike aliyeitwa Nomsa ambapo watoto hao walisoma katika shule ya msingi ya Mazimbu Morogoro wakati huo watoto walikuwa wakiishi na baba yao katika kambi ya wakimbizi na kwenda kwa mama yao siku jumamosi kusalimia kitongoji cha Manyata. Alisema Bi Naomi.
Taarifa za kuondoka kwa watoto hao na baba yao kwenda Afrika ya Kusini, Miriam Chimile alizipata baada ya wiki moja kutokana na kupata taarifa ya kugongwa kwa watoto wa wakimbizi katika kambi ya Mazimbu ambapo alitumwa kaka yao kwenda kuangalia ni mtoto gani ambaye amegongwa na kupata taarifa za kuondoka kwa wakimbizi hao.
Naomi akimnukuu maremu mdogo wake Miriam Chimile alisema kuwa kitendo hicho hakikumdhirisha kwa kuondoka na watoto bila ya kumpa taarifa kwani yeye (Miriam) hasingeweza kumzuia kuondoka na watoto hao ambapo kitendo hicho kilimsikitisha sana na kudai kuwa kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kufahamu sehemu ambayo watoto wake wanaishi na kupata mawasiliano ya huko Afrika ya Kusini. Alieleza.
Baada ya Miriamu Chimile kupata maladhi ya ugonjwa wa kifua kikuu na kukata tamaa ya kuishi duniani alitoa usia kwa dada yake Naomi na kusema kuwa kama atafanikiwa kuwaona watoto wake atamshukuru mungu na kama atafariki dunia ataomba watoto wake waonyeshwe kabuli lake. Alisema Naomi.
Naomi akimnukuu mdogo wake Miriam Chimile wakati akiwa katika hospitali ya Bwagala ya Turiani alisema kwa kumuuliza swali kwa kusema kuwa dada mimi nakufa sasa nitafanyaje juu ya watoto wangu ? ambapo aliweza kumjibu mdogo wake kwa kusema kuwa kama damu yako mzito hao watoto watakuja kwa uwezo wa mwenyezi mungu na malaika wake.
“Kulikuwa na malumbano kati ya mjomba wake na Miriamu juu ya kuondoka kwa watoto hao kwenda Afrika ya Kusini na baba yao Lebonang Christopher Mpetwane ambapo Miriam hakuwa na kipingamizi juu ya kuondoka nao watoto".Naomi alimnukuu mdogo wake.
Aliongeza kwa kueleza kuwa alielekeza lawama kwa mzazi mwenzake kwa kushindwa kumpata taarifa ya kuondoka na watoto hao kwani yeye hasigekuwa na kipingamizi kwani kitu ambacho alikuwa akihitaji kupata kwa elimu kwa watoto wake na kuwa kosa ambalo alilifanya ni kuondoka bila ya kutoa taarifa basi”.
Akielezea maisha yake Naomi Godwin alisema amekuwa akiishi katika mazingira magumu kwani katika kaya yake kumekuwa na familia zaidi ya watu kumi hivyo kushindwa kufanya zitihada za kuwasiliana na watoto wa mdogo wake ambapo wapo Afrika ya Kusini kutokana na kipato kidogo anachopata na kuomba serikali kuweza kumsaidia namna ya kuweza kuonana na watoto hao japo kwa kumleta nchini hata kwa wiki moja.
“Nimekuwa na familia kubwa sana kwani marehu mdogo wangu Miriam Chimile ameniachia watoto watano na mimi mwenyewe nina watoto watano”. Alisema Naomi.
Naomi alisema amekuwa akipata taarifa za Nomsa na kaka yake Nhanhla waliopo Afrika ya Kusini kupitia kwa watoto wa wakimbizi wa kijiji hicho ambapo wamekuwa wakitoa taarifa juu ya watoto hao na kuongeza kuwa kikwazo kikubwa kipo kwa baba yao kwani amekuwa na tabia ya kuwazuia kuja Tanzania kuonana na familia mama yao pamoja na ndugu.
Naomi alisema katika uhai wake Miriam Chimile ameacha watoto saba ambao amezaa na wanaume tofauti ambapo aliwata watoto hao kuwa ni Mapenzi Athumani (35), Tatu Masudi (30), Sakina Masudi (27), Nomsa Lebonang Christopher Mpetwane, (24) Nhanhla Lebonang Christopher Mpetwane (Nhanhla) (26), Masha Dyagule (20) na Quween George (18).Chanzo:MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment