Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia AcksonNaibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amewasimamisha wabunge wawili wa Viti Maalum Chadema baada ya kupatikana na hatia ya kusema uongo na kutoa taarifa ambazo hazina ukweli bungeni.
Dk Tulia amemsimamisha Suzan Lyimo kutohudhuria vikao vitano na Anatropia Theonest kutohuduria vikao vitatu baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyowasilishwa bungeni leo iliyokuwa ikieleza kuhusu tuhuma za wabunge hao.

0 comments:
Post a Comment