BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WENYE SIMU FEKI WAFANYA MAJARIBIO WENYEWE KWA KUZIZIMA NA KUWASHA TANZANIA.

MAMLAKA ya Mawasiliano (TCRA), imeeleza kuwa wananchi wamekuwa wakizizima na kuziwasha mara kwa mara simu feki zilizo katika mitandao ya mawasiliano nchini, ingawa matumizi yake kwa ujumla yamepungua.

Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi alieleza kuwa katika mazungumzo na Nipashe, jijini Dar es Salaam juzi kuwa wananchi wamekuwa wakiziwasha simu feki na kuzijaribu mara kwa mara ili kufahama kama zimeshazimwa tayari ama la.

Mungi alikuwa akizungumza na Nipashe kuhusu uzimawaji wa simu hizo ifikapo Alhamisi.

“Takwimu zetu zinaonyesha simu feki zimepungua sana, wananchi wameelimika, maeneo mengine unakuta kati ya watu 200 wanaotumia siku hakuna simu feki au ipo moja,” alisema Mungi.

Alisema changamoto kubwa iliyobaki ni wananchi kutoamiani kama kweli zitazimwa.

Alisema hali hiyo inawafanya watu wenye simu feki ambao walishaacha kuzitumia, waziwashe simu zao kwa muda na kuzizima. Lakini “mpango wetu uko pale pale," alisema Mungi. "Simu feki lazima zizimwe Juni 16 mwaka huu, na tunaandaa taarifa ya kina juu ya tukio hili.”
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: