BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAISHA YA NYUMBU HIVI NDIO YALIVYO NDANI YA HIFADHI YA WANYAMA

Na Ng’oko Innocent.
NYUMBU (Wildebeest) ni Mnyama mkubwa anayepatikana Afrika tu katika maeneo ya Savana na kuna aina mbili za nyumbu ambao wana rangi yeusi na mng'ao wa bluu au kahawia. Dume na jike wana pembe zenye umbo la ng'ombe na hupendelea kula majani mafupi.

Nyumbu anatajwa kuwa ni mnyama mwenye uwezo mdogo wa kufikili na katika maisha yake ya kila siku hupenda kujichanganya na wanyama wengine kama pundamilia, nyani wakubwa na baadhi ya ndege wakiwemo yangeyange kama kinga ya kumwezesha kumwepusha au kumshitua na maadui.

Maajabu ya Nyumbu hawana utamduni wa kusaidiana pindi mmoja wao anapokamatwa na adui, na wanapofukuzwa na adui kila mmoja hutumia jitihada binafsi za kujiokoa mwenyewe lakini ni mara chache mtoto anaposhambuliwa na wanyama wadogo kimaumbile kama chui ama fisi hupambana naye kuokoa maisha ya mwanaye.

Kwa kawaida Nyumbu wenye mng'ao bluu au kahawia wanapatikana zaidi Afrika ya Mashariki katika nchi za Tanzania na Kenya na nyumbu wa maeneo haya ni wakubwa kwa umbo, pia nyumbu hupatikana upande wa kusini mwa Afrika katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini, Sawaziland na nchi ya Angola.

Kundi moja la Nyumbu linakadiliwa kuwa na nyumbu 300,000 hadi 400,000 na wakati wa kuhama huambatana na wanyama wengine wakiwemo pundamilia, na nyumbu ana uwezo wa kuishi miaka 20 ingawa wengi wao ni waoga sana licha ya kuwa na sura za kutisha.

Si Nyumbu wote wanatabia ya kuhamahama na nyumbu wenye mng'ao bluu au kahawia ndiyo wenye utamaduni wa kuhamahama kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine na huwafanya kuwa kivutio kikubwa kwa watalii wakati wa msimu wa kuhama na kwa kawaida wana uzito wa kg 250.

Nyumbu weusi kwa kawaida wana uzito wa Kg 180 tu na hawana tabia ya kuhamahama hovyo na huwa na eneo maalum kwajili ya malisho na nyumbu dume hupenda kutawala eneo wanaloishi ,ni jambo la kawaida kwa nyumbu dume wasio na majike hutengeneza kundi lao na ni kawaida kwao kuzurula hovyo.

Nyumbu hawapendi maeneo ambayo ni makame sana au yenye unyevunyevu mwingi na wanapendelea zaidi katika maeneo yenye uwanda wa nyasi fupi na vichaka vya hapa na pale(Savana) .

Wanyama hao aina ya Nyumbu hususani wenye mng'ao bluu au kahawia kwa kawaida huishi katika makundi makubwa sana na wanapatikana zaidi katika mbuga ya wanyama ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania, hifadhi ya Taifa ya Maasai Mara nchini Kenya pamoja na mbuga ya wanyama ya Taifa ya Liuwa Plain nchini Zambia na madume hutawala kwenye kundi na madume yasiyo na majike hutengeneza kundi lao.

Ukiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Masai Mara Nchini Kenya si kawaida sana kuona kundi kubwa la Nyumbu wenye mng'ao bluu au kahawia wakihama kutokana na shughuri za ufugaji,kilimo na mvua zisizo na uhakika kuwaathili nyumbu hao.

Na nyumbu huhama kutokana na kutafuta malisho ya Uhakika,maji na wakati mwingine hulazimika kuwakimbia adui wanapozidi katika eneo husika na kwa Tanzania zoezi la Nyumbu kuhama huonekana vizuri zaidi na kuwa kivutio kwa watalii na wana uwezo wa kukimbia Km 80 tu.

Kwa kawaida Nyumbu huzaliana wakati mvua zinapoishia na ndama wa nyumbu huwa na uzito wa kg 21 muda mfupi baada ya kuzaliwa na katika hifadhi ya serengeti wastani wa nyumbu zaidi ya 8000 huzaliwa kila siku na nyumbu karibu wote ambao huhamia kwa muda katika hifadhi ya Masai mara huzaliwa Tanzania.

Ni jambo la kawaida kwa nyumbu ndama kuwa na uwezo wa kuongozana na kundi la nyumbu muda mfupi baada ya kuzaliwa na ni utamaduni kwa nyumbu kuwa hawana muda wa kulemba wa kuwatunza nyumbu ndama na inakadiliwa zaidi ya nyumbu 200,000 hufa wakati wa zoezi la kuhama la mwezi Julai na Oktoba na Tai (VOLTURE) hula mizoga hiyo kwa 70%.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: