BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AMSHUSHIA MKONG'OTO DIWANI WA CCM.


Shinyanga. Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Itubamilo Halmashauri ya Shinyanga, amedaiwa kumpiga diwani wa viti maalumu (CCM) Kata ya Didia, Mengi Charles na kumjeruhi.

Tukio hilo lililotokea wakati wakiwa kwenye kikao cha kamati ya maandalizi ya harusi, limesababisha diwani huyo kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

Akizungumza akiwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, diwani huyo amesema walipokuwa katika kikao hicho, mwalimu huyo alikuwa amelewa na kuanza kufanya fujo.

“Ilipotolewa hoja na wajumbe kuhusu mapambo, mwalimu alitaka apewe kazi hiyo kwa madai ana mtu wa kufanya shughuli hiyo, lakini wajumbe walimtaka mmlete ndipo tatizo lilipoanzia na kusababisha vikao kutoisha. 


Saa mbili usiku baada ya kikao kuisha tulitoka nje ndipo alinivamia na kunipiga,”amesema diwani.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: