BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YAZUIA BENKI KUTOZA TOZO YA 18% YA VAT YA MIAMALA YA WATEJA.

Serikali imezuia benki kupandisha viwango vya tozo katika miamala yake na kuelekeza gharama hizo kwa wateja wao.

Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa asilimia 18 ya VAT mpya iliyopitishwa kwenye miamala ya benki inahusisha gharama zilizokuwa zikitozwa na benki hizo kwa wateja wao lakini serikali ilikuwa haipati chochote.

Kidata amesema kuwa Benki Kuu imeelekezwa kudhibiti benki hizo kwa kufanya ujanja wa kuongeza makato kwenye miamala ya wateja wao wakati wakijua fika kuwa hilo si lengo la kodi hiyo mpya.

Ameelekeza kuwa kiwango cha kodi kinachotozwa kwenye miamala hiyo kinatakiwa kubaki kama mwanzo lakini serikali itakata kodi yake ya asilimia 18 na kodi nyingine zilizopo kwa mujibu wa sheria

Kwakifupi ni kwamba Serikali imezuia Benki kupandisha viwango vya tozo katika miamala yake na kuelekeza gharama hizo kwa wateja wao.

Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa asilimia 18 ya VAT mpya iliyopitishwa kwenye miamala ya benki inahusisha gharama zilizokuwa zikitozwa na benki hizo kwa wateja wao lakini serikali ilikuwa haipati chochote.


Kidata amesema kuwa Benki Kuu imeelekezwa kudhibiti benki hizo kwa kufanya ujanja wa kuongeza makato kwenye miamala ya wateja wao wakati wakijua fika kuwa hilo si lengo la kodi hiyo mpya.

Ameelekeza kuwa kiwango cha kodi kinachotozwa kwenye miamala hiyo kinatakiwa kubaki kama mwanzo lakini serikali itakata kodi yake ya asilimia 18 na kodi nyingine zilizopo kwa mujibu wa sheria.


Imeandikwa kwa msaada wa dau:Ahmad Issa Michuzi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: