BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI AMTEUZI AUGUSTINO MREMA KUWA MWENYEKITI BODI YA TAIFA YA PAROLE.


Augustino Lyatonga Mrema 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Katika uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Mwenyekiti wa Chama cha TLP Taifa, Mhe. Augustino Lyatonga Mrema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole. Miezi kadha iliyopita Mrema alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akimuomba Rais Magufuli ampe kazi yeyote kwenye serikali yake ili amsaidie kutumbua majipu.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Mhe. Augustino Lyatonga Mrema.


Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: