BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIGARA, MSHUMAA VYANZO VYA MOTO KUTEKETEZA VIBANDA 500 VYA WAFANYABIASHARA MWANZA.

Sengerema. Moto umeteketeza vibanda zaidi ya 500 vya biashara visiwani Kabiga na Migongo wilayani Serengeti Mkoa wa Mwanza.

Moto huo umetokea katika matukio mawili tofauti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema leo kuwa katika Kisiwa cha Kabiga Kata ya Maisome zaidi ya vibanda 300 viliteketea Alhamisi wakati wafanyabiashara walipokuwa wakigawana mafuta ya petroli yanayodaiwa kuibwa.

Amesema mmoja wa wafanyabiashara hao aliagusha kipande cha sigara kilichowashwa ndipo moto ulipolipuka. Amesema katika Kisiwa cha Migongo Kata ya Maisome, zaidi ya vibanda 200 viliteketea jana usiku chanzo kikiwa ni mshumaa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: