BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UNDANI WA UANZISHWAJI WA KUNDI LA AL SHABAAB LIMETOKANA NA MUUNGANO WA MAHAKAMA NCHINI SOMALIA

Jina la Kikundi Kinachoitwa cha 'kigaidi' cha Harakat Al Shaabab Al Mujahideen ("Mujahideen Youth Movement" or "Movement of Striving Youth"), maarufu kama Al Shaabab si jina la kisomali ila ni jina la Kiarabu hasa likimaanisha 'Vijana wenye kupigana Vita Vitakatifu'.

Ukumbuke kwamba lugha aghalabu hutumika kwa utashi ama mazingira yake na ndio maana wao wanaamini wanapigana 'vita vitakatifu' ilihali wale wa magharibi wakiwaita 'magaidi' na ndio maana pia wakati wewe ukiwaita 'wanaojilipua' (suicide bombers ) wao hujiita 'wafia dini' (martyrs) na kiukweli huwa na hamu sana siku yao ifike haraka kwenye ratiba wakiamini wanakufa kama washindi na wenye thawabu kuu kwa Subhan Allah

Jina la Kikundi Kinchoitwa cha 'kigaidi' cha Harakat Al Shaabab Al Mujahideen maarufu kama Al Shaabab si jina la kisomali ila ni jina la Kiarabu hasa likimaanisha 'Vijana wenye kupigana Vita Vitakatifu'.


Kundi hilo liliibuka kama tawi la vijana la muungano wa mahakama za kiislmau ambao baadaye ulivunjika mwaka 2006, wakati ilipopigana na wanajeshi wa Ethiopia waliokuwa wameingia nchini Somalia kuunga mkono serikali iliyokuwa dhaifu.

Ingawa wengi wanadiriki kufananisha Al Shaabab na Uislamu, wakiita Al-Shabaab inajulikana kama kundi la wanamgambo wa Kiislamu kupigana kwa ajili ya nafsi ya Somalia, Hitimisho la Mkutano wa wasomi wa Kiislamu walitoa Fatwa dhidi ya al -Shabaab , wakisema, ‘ Hawafuati uislamu ipasavyo wanavyofanya siyo uislamu haipaswi waungwe mkono”, Fatwa mara nyingi zinazohusiana na vitisho vya kuuawa au hukumu.

Hadi sasa inasemekana kuwa na wapiganaji wenye silaha zaidi ya 10,000. Mbunge Hussein Bantu wa bunge la Somalia anasema kundi hilo limejaa raia wa kigeni, wengine kutoka Pakistan na Afghanistan, na kwamba raia wa Somalia wanachama wa kundi hilo ni wachache. 


Maafisa nchini Marekani wanaamini kuwa wapiganaji wa Al Qaeeda ambao hawajahusina sana na mashambulizi nchini Afghanistan na Pakistan kufuatia mauaji ya kiongozi wao,Osama bin Laden, wapiganaji wake wengi wanakwenda kutafuta hifadhi nchini Somalia.

Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti, wa miji mikubwa, kwani lililazimika kuondoka katika mji mkuu Mogadishu, mwezi Agosti mwaka 2011 na pia kuondoka katika mji wa bandarini wa Kismayo mwezi Septemba mwaka 2012.


Kismayo ulikuwa ngome muhimu kwa kundi hilo, ambao ulikuwa unawezesha bidhaa kuwafikia wapiganaji wa kundi hilo pamoja na kuwatoza watu ushuru kwa shughuli zao. Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti, wa miji mikubwa, bado linakita mizizi katika maeneo ya vijijini ambako wanajiimarisha na kuendelea na operesheni zao

Al shaabab walijiunga rami na mtandao wa kigaidi wa Al Qaida mnamo mwaka 2012 na hasa katika kutafuta 'ruzuku zaidi' (kiongozi wake Osama Bin Laden aliuawa mwezi Mei mwaka huu wa 2011).


Kundi hilo limeweka sheria kali za kiisilamu katika maeneo ambayo linadhibiti ikiwemo kupigwa kwa mawe hadi kufa wanawake wanaodaiwa kufanya uasherati pamoja na kuwakata wezi mikono (SHARIA).

Tishio la al-Shabaab lilikumba Somalia baada ya muda mrefu wa kutokuwepo na serikali thabiti kwa miaka takribani 25 sasa. Serikali ya mwisho iliyokuwa thabiti iliongozwa na rais Mohammed Siad Barre aliyetimuliwa madarakani mwaka wa 1991. 


Tangu hapo yeyote ambaye ameongoza Somali iiwa ni pamoja na mawaziri wamekua katika hali ya hofu kuu kutokana na al shaabab kiasi cha kuwafanya kutodumu madarakani kwani wanashindwa kuoanga mipango endelvu ya maendeleo na hivyo kufanya hali ya maisha na hasa njaa kuendelea kuikumba somali kutokana na kugubigwa na matishio ya mara kwa mara ya kikund hiki ambapo pale unapodhani kimekufa ndio HUIBUKA KWA NGUVU KUBWA

Wadadisi wanaamini kuwa al-Shabab limeanza kufanya mashambulizi ya kuvizia baada ya kushindwa na majeshi ya Muungano wa Afrika wanaotumia nguvu dhidi yao. Kiongozi wa Kundi hilo, Ahmed Abdi Godane ndiye kiongozi wa kundi hilo.


Anajulikana kama Mukhtar Abu Zubair, na anatoka katika jimbo la Somaliland si aghalabu kumuona hadharani ukitazama picha ya kwanza na ya pili utagundua kwamba hata viatu vyao ni kama kandambili tu na pengine hudiriki hata kuwa pekupeku huku akiwa ameshika silaha KALI YA AK 47.

Kuna nini nyuma ya pazia? nani wafadhili wa AL SHAABAB??? kuna propaganda nyingi sana nyeusi nyeupe na kijivu kuhusu Al shaabab na HII NAYO NI SIRI YA JICHO LA TATU.

Moja ya ajenda kuu duniani kwa sasa.........Ni vizuri tukaelewa mujahidina hawa wanapata wapi nguvu zao, na kwa nini imekuwa vigumu kwa majeshi ya AU na Marekani kuwang’oa
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: