VYETI KUWAPONZA WATUMISHI WA SERIKALI 3600 KUKOSA MISHAHARA MWEZI WA NANE TANZANIA
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Tanzania wanaochukua fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakionyesha vyeti vyao.Picha ya maktaba
Pwani. Uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma mkoani Pwani kuwaweka watumishi 3,600 kwenye hatari ya kukosa mishahara ya Agosti mwaka huu baada ya kubaini mapungufu katika taarifa zao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angela Kairuki amesema kati ya hao, watumishi 3,569 taarifa zao za kielimu hazionekani,36 wana zaidi ya miaka 60 lakini wako kazini badala ya wamestaafu, sita akaunti zao hazitambuliki na 21 vyeo vyao havijabainishwa.
Amesema hivyo haitawezekana kulipwa mishahara kuanzia Agosti hadi hapo mapungufu ya taarifa zao zitakaporekebishwa. Akizungumza na watumishi wa umma Pwani, Kairuki amesema Bagamoyo ina watumishi 2,175 wenye taarifa zenye upungufu, Rufiji (912), Kibaha Mji(465), Mkuranga (21) Kibaha Vijijini (14), Mafia na Kisarawe (8).
0 comments:
Post a Comment