WATALII WASHIKWA NA HOFU BAADA YA NYANGUMI MKUBWA ALIPOIBUKA MAJINI KARIBU NA BOTI YAO NA KUYUMBA
Ni mandhari ya kupendeza sana... Utadhani maonyesho..
Ni wakati nyangumi mmoja aliporuka juu kutoka ndani ya maji ,mita chache tu kutoka mahali boti moja ya watalii ilipokuwa inapita.
Nyangumi kumi na wawili walikuwa wakiogolea karibu na ufuo wa pwani ya kaskazini mwa Sydney nchini Australia.
Ulikuwa wakati wa msimu wa nyangumi hao kuhama kutoka sehemu moja ya bahari ya Australia hadi nyengine.
John Goodridge ni mmoja waliokuwa wakitazama mwenendo wa nyangumi wakati alipopiga picha hiyo yakuvutia akiwa katika boti nyengine umbali wa mita 500.
‘Kwangu mimi , lilikuwa tukio la kufurahisha, na kuchekesha lakini najua kwao yaaani watalii hao lilikuwa tukio la kushtusha kweli!
Kwani wakati nyangumi huyo alipofanya hivyo boti lao liliyumba utadhani ni kifiniko cha chupa baharini' John Goodridge ameelezea
Nyangumi huyo alikuwa na uwezo ha kulitosa boti hilo na pamoja nayo maisha ya makumi ya watalii ,mnyama huyo alikuwa ni mkubwa sana.
Maelfu ya nyangumi wanaelekea Queensland ambako msimu ni baridi zaidi huko.
Viumbe hao wa kuvutia wanatarajiwa kurudi tena bahari ya Antarctic kutoka Septemba hadi Novemba.
"Mara nyingi nyangumi huwa wanashangaa kuona boti baharini lakini ni nadra kwamba wataziandama na kuruka ruka karibu ya vyombo vya baharini,"BBC
0 comments:
Post a Comment