BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

URENO YAINGIA NUSU FAINALI YA KOMBE LA UERO 2016 KWA MBINDE BAADA YA KUILAZA POLAND UFARANSA.

 
Timu ya taifa ya Ureno imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Euro 2016 baada ya kuiondosha mashindano timu ya Poland usiku wa June 30 2016m kwa changamoto ya mikwaju ya penalti ya bao 5-3 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Stade Velodrome jijini Marseille Ufaransa.

Ureno iliibuka vidume katika mchezo huo baada ya kumalizika kwa sare ya bao 1-1 na kuongezwa dakika 30 na kuufanya mchezo huo uchelezwe kwa dakika 120.

Poland ndio iliyoanza kupata bao dakika ya pili lililofungwa na mshambuliaji, Robert Lewandoski huku Ureno wakifanya kazi ya ziada ya kugomboa bao hilo kupitia kwa, Renato Sanchez dakika 33.

Kutokana na matokeo hayo timu ya taifa ya Ureno imefuzu kutinga hatua ya nusu fainali huku ikisubiria mshindi katika mchezo wa robo fainali kati ya Wales ama Ubelgiji.

timu ya taifa ya Ureno imekutana na Poland katika mechi 11 na kufanikiwa kuibua videdea mara tano ikitoa sare mara tatu na kupoteza michezo mitatu tangu October 16 mwaka 1976.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: