BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DK JUMA MWAKA AITUNISHIA MISULI SERIKALI BAADA YA KUFUNGIWA, SASA KUBURUZWA MAHAKANI KWA UKAIDI.


Naibu Waziri wa Afya Dk.Hamisi Kigwangalla, ametoa saa 24 kwa Jeshi la Polisi kumtia ndani Dk Juma Mwaka na kumfikisha kortini, kwa kukiuka amri ya Baraza la Tiba Asili nchini ya kusitisha shughuli zake.

Pamoja na mambo mengine, Dk Mwaka anatuhumiwa kuendesha shughuli za utabibu wa kidaktari wa tiba za kisasa, tofauti na masharti ya leseni yake ya tiba asilia.

Aidha, amekutwa na kukutwa na shehena ya dawa za tiba asili, licha ya kazi zake kupigwa marufuku na baraza la tiba asili.


Dk.Kigwangalla ameibuka tena kwenye kiliniki hiyo iliyoko Ilala Bungoni Jijini Dar, kufanya ukaguzi wa kinachoendelea ambapo hivi sasa imebadilishwa jina.

Dk Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza katika kiliniki hiyo kama alivyowahi kufanya mara baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.

Tofauti na ziara yake ya awali, safari hii Dk Kigwangalla ilibidi alisubiri kupata kibali cha OCD Polisi wa eneo hilo kabla ya kuingia ndani ya jengo hilo.


Hivi karibuni Baraza la Tiba Asili nchini, lililopo chini ya Wizara ya Afya, liliifutia leseni ya tiba asilia kliniki hiyo kwakiuka masharti ya baraza hilo.


Maoni:
Dk Mwaka acha kuivimhia serikali.Fuata masharti yako tu,ili umalize kifungo na usonge mbele.Enzi za ujanja ujanja zimepita.Kazi nzuri sana serikali:

 Dkt Hamisi Kigwangalla Ummy Mwalimu Nsachris Mwamwaja Zamaradi Kawawa Gerson Msigwa
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: