HAYA NDIO MAISHA YA KOBE YALIVYO NA MAAJABU YAKE UTAYAPENDA TU.
Na Geofrey Chambua
Kobe ni mnyama jamii ya Reptilia ambaye kwa kumtazama tu lazima ujiulize maswali mengi.Kitendo chake cha kuficha kichwa, mwendo wake na gamba lake gumu!!
1. Licha ya chakula chake kuwa nyasi, magugu na matunda lakini KOBE hana meno
2. Ni kweli kwamba gamba la kobe ni gumu sana kama unavyoliona ambapo pia humsaidia kuhimili shuruba mbalimbali, ukithubutubu kuligusa gamba hilo hata kwa unyoya wa kuku, KOBE anatambua kuwa ameguswa Ana hisia kali sana!!
3. Licha ya kwamba KOBE hawezi asilani kuogelea, ukweli ni kwamba KOBE anaweza kuzama na kuishi bila kuvuta pumzi kwa muda mrefu sana akiwa gubigubi majini. Ukimwondoa Nng’e kobe anafuata kwa uwezo wa kuishi muda mrefu bila kupumua
4. KOBE wa sasa unaowafahamu wanaweza kuishi hadi miaka mia moja!!
5. Kobe mkubwa kabisa duniani ana uzito wa kilogram mia saba.. hii inamfanya kuwa reptilia mzito kupita wote!!
6. Sina hakika sana lakini ninashawishika kuamini kwamba asili ya wasiofunga kuitwa KOBE ni kwa sababu wasiofunga, hasa wale wasiotaka kuonekana kuwa hawajafunga, hula kwa kujifichaficha km afanyavyo kobe. Kobe anaweza kula huku kichwa chake kikiwa ndani ya gamba lake, na hivyo kutoweza kuonekana.
0 comments:
Post a Comment