MCHUNGAJI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUNGA KWA SIKU 30 AKIJARIBU KUJIPAMBANISHA NA YESU KRISTO
Mchungaji wa South Africa Alfred Ndlovu (44) amefariki baada ya kufunga usiku na mchana kwa siku thelathini akitaka kuvunja rekodi ya Yesu Kristu aliyefunga siku Arobaini usiku na mchana bila kula wala kunywa kitu chochote.
Mchungaji Alfred aliondoka nyumbani kwake tarehe 17/6/2016 na kuelekea nyikani kwa ajili ya kufunga na kuomba, huku akiweka nia kwa Mungu na kujitenga na anasa za ulimwengu. Alikuwa peke yake nyikani na maiti yake ilionwa na mpita njia aliyetoa taarifa polisi.
0 comments:
Post a Comment