BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDEGE MBILI ZA KAMPUNI YA NDEGE YA TANZANIA (ATCL) ZIKIWA HATUA YA MWISHO NCHINI CANADA



Mafundi wa kampuni ya ndege ya Bombadier ya Canada wakipaka rangi moja ya ndege mbili za Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) katika karakana ya kampuni hiyo nchini humo. Ndege hizo zinatarajiwa kutua nchini Septemba mwaka huu.


KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL) inatarajia kuingiza nchini ndege zake mpya mbili mwishoni mwa mwezi ujao.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, ujio wa ndege hizo utaleta mapinduzi makubwa kihuduma na kiutendaji kwa kampuni hiyo, huku shukrani zaidi zikielekezwa kwa Rais John Magufuli kwa jitihada zake za kufufua rasmi ATCL.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Patrick Itule alisema Dar es Salaam jana kuwa ujio wa ndege hizo utairejesha kampuni hiyo kwenye biashara ya ushindani dhidi ya kampuni nyingine za ndege hapa nchini.

Ndege hizo zinazotengenezwa na kampuni ya Bombardier ya nchini Canada zinatarajiwa kuingia nchini wiki ya tatu na ya nne ya Septemba, mwaka huu, zikipishana kwa wiki moja.

“Baada ya ujio wa ndege hizi hatuoni tena sababu ya sisi kukwama, tutakuwa tumeingia rasmi kwenye biashara ya ushindani kwa kuwa changamoto kubwa ya uhaba wa ndege ambayo imekuwepo kwa miaka kadhaa sasa itakuwa imeanza kutatuliwa,’’ alibainisha Itule.

Alisisitiza kuwa ATCL haitakuwa tayari kuwavumilia wafanyakazi watakaoshindwa kuendana na kasi ya mabadiliko ya sasa.

Alisema ATCL tayari imeunda kikosi kazi kinachosimamia masuala mbalimbali, likiwemo la mafunzo ya watendaji wake mbalimbali ili kuendana na matakwa ya biashara hiyo kwa sasa.

Akizungumzia uwezo wa ndege hizo, Ofisa Biashara wa ATCL, Josephat Kagirwa alisema zina uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na kwamba ujio wake utaongeza njia za kusafiri kwa kampuni hiyo kutoka njia mbili za sasa hadi kufikia njia zaidi ya kumi.

“Tutakuwa na madaraja mawili, yaani daraja la uchumi litakalohusisha abiria 70 na daraja la biashara litakalohusisha abiria sita kwa kila ndege,” alisisitiza.HABARILEO.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: