BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI WAFICHUA SIRI YA MFUNGWA SUGU BILIONEA ALIYEKUWA AKIISHI MAISHA YA KIFAHALI GEREZANI


Polisi nchini Paraguay wamegundua seli ya kifahari katika gereza la wafungwa sugu nchini humo Tacumbu.

Seli hiyo ilikuwa ya mfungwa mmoja ambaye ni kiongozi wa genge la ulanguzi wa mihadarati.

Katika seli hiyo ya kipekee yenye vyumba vitatu polisi waligundua mlikuwa na sebule, maktaba, jiko na chumba cha kutizama televisheni.

Mlanguzi wa mihadarati raia wa Brazil Jarvis Chimenes Pavao ndiye aliyekuwa akiishi humo na mfungwa yeyote aliyetaka kuishi naye humo alitozwa kodi ya dola elfu tano pesa taslim.

Lakini kwanini waishi humo ?

Mlikuwa na viti vya kifahari, yaani mwenyeji angeweza hata kutazama vipindi ya runinga, video , angeweza kuoga maji ya moto

Kuta yake ilikuwa imewekwa matofali ya kisasa na ya kuvutia.

Uchunguzi umeanza kubaini ni maafisa waga katika gereza hilo waliomruhusu mlanguzi huyo wa mihadarati kuishi maisha hayo ya kifahari humo gerezani.


Sadfa ni kuwa mle ndani mlikuwa na video moja iliyokuwa na simulizi ya maisha ya mlanguzi hodari wa mihadarati kutoka Colombia Pablo Escobar.

Escobar ambaye aliuawa mwaka wa 1993 alikubaliana na viongozi wa idara ya magereza nchini Colombia kuwa atakubali kutumikia kifungo chake gerezani ilimradi tu aruhusiwe kuijenga seli atakamoishi.

Wafungwa wenzake wamehuzunishwa na ugunduzi huo wa polisi ambao wanadai umewapokonya bwana mkarimu sana humo gerezani.

Mmoja wa wafungwe wenza bwana Antonio Gonzalez amenukuliwa akisema kuwa alikuwa maarufu sana ,na aliwapenda wote aliokutana na kujumuika naye.

''Alikuwa bwana mcheshi sana ''

Mfungwa huyo tajiri wa kupindukia amehamishwa hadi katika gereza lililoko karibu na mji mkuu wa Asuncion.

Polisi waligundua seli hiyo ya kipekee katika gereza hilo la Tacumbu baada ya kudokezewa kuwa kulikuwa na mtu aliyeagiza aletewe bomu mle ndani.

Yamkini rais huyo wa Brazil Chimenes Pavao ambaye alikuwa anatarajiwa kukamilisha kifungo chake cha miaka minane gerezani hapo mwakani hakutaka arejeshwe Brazil, kwa hivyo alikuwa amepanga njama aletewe bomu ambalo angelitumia kulipua ukuta wa gereza hilo na kutoroka.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: