BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TASWIRA YA MATUKIO MAONYESHO YA WAKULIMA KANDA YA MASHARIKI UWANJA WA MWL JULIUS NYERERE NANE NANE MOROGORO

Waziri mkuu Kassimu Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi mkuu wa banda la magereza, Msepwa Omari wakati alipotembelea katika vipando vya banda hilo katika ufunguzi wa maonyesho ya wakulima Nane Nane kanda ya mashariki katika uwanja wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere Morogoro.
Balozi wa Indosia nchini Tanzania, Zakaria Anshar akikabidhiwa zawadi ya shuka na Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushiriki, Rosemary Buge wakati balozi huyo alipotembelea banda la halmashauri ya wilaya ya Handeni katika maonyesho ya wakulima Nane Nane kanda ya mashariki yanayofanyika uwanja wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere.
Elias Jonas na Catherine Mumwi wakipalilia mazao jamii ya mikunde katika vipando vya banda la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Ilonga (ARI ILONGA) katika maonyesho ya wakulima kanda ya mashariki yanayoanza leo agosti mosi uwanja wa Mwl Julius Nyerere Morogoro.
Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Jaji mstaafu, Damian Lubuva akizungumza jambo na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika maonyesho ya wakulima Nane Nane kanda ya mashariki yanayofanyika kwenye uwanja wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere Morogoro.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: