MAANDAMANO YA UKUTA YAYEYUKA KESHO OKTOBA MOSI
Mwenyekiti wa Chadema akitangaza kuahirisha mikutano na maandamano yaliyopangwa kuanza kesho nchi nzima kwa jina la Ukuta, akisema safari hii hautakuwa na tarehe maalumu. Picha na Boshe Nyanje
Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahirisha tena mikutano na maandamano nchi nzima iliyokuwa na jina la Ukuta safari hii bila kutaja tarehe nyingine.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema hawataji tarehe nyingine ili kukwepa maandalizi ya Serikali yanayoweza kuwadhuru wanachama wao.
Ametaja sababu ya kuahirisha Ukuta akisema ni kukosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wa dini waliowaomba waahirishe ili wakazungumze na viongozi wa Serikali.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment